Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wachungaji wa kondoo tu, walijali

  Katika uwanda ambapo Daudi alikuwa akichungia kondoo, wachungaji waliokuwa wakikehsa usiku, waliongea habari ya ahadi ya Mwokozi, wakaomba sana ili apate kuja. Ndipo malaika wa Bwana akawajia, akawaambia, “Msiogope, maana nawaletea habari njema, itakayokuwa furaha kwa watu wote. Maana amezaliwa Mwokozi kwa ajili yeny leo katika mji wa Daudi, naye ndiye Yesu Kristo Bwana.”TVV 22.5

  Kwa maneno haya, njozi ya utukufu ikajaza mawazo ya wachungaji waliokuwa wakisikiliza. Mkombozi amekuja! Kuja kwake kutakuwa na uwezo, na ukuu, na ushindi. lakini malaika waliwatayarisha ili wamtambue Mwokozi katika mahali hafifu alikozaliwa. “Mtamkuta mtoto amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini.”TVV 22.6

  Mjumbe wa mbinguni ametuliza mioyo yao, na hofu zao. Amewaonyesha namna ya kumwona yesu. amewaonyesha muda wa kumfahamu. Halafu uwanda wote ukaangazwa na nuru ya majeshi ya Mungu. Nchi ikanyamaza kimya, na mbingu ikatulia ili kusikiliza wimbo:“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”TVV 22.7

  Laiti watu wangeweza kuuelewa wimbo huo leo! Kama ungeimbika ilivyo ungeweza kuenea mpaka mwisho wa wakati, na ungetoa mwangwi wake mpaka kona za nchi.TVV 23.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents