Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo alivunja mtengano wa matabaka

    Yesu alianza kazi yake kwa njia ya kuwahurumia watu Wakati alikuwa mtiifu wa amri za Mungu, alikemea unafiki wa Mafarisayo; naye alijaribu kuwatoa katika vifungo vya sheria walivyofugiwa na Mafarisayo. Alikuwa akitaka kuvunja mtengano wa matabaka ya watu tofauti katika jamii. Alitaka awalete watu katika hali ya umoja kama watu wa jamaa moja.TVV 77.3

    Yesu alishambulia hali ya ubinafsi, walakini yeye alikuwa mtu wa kushirikiana na watu wote. Alikuwa mkarimu kwa watu wa hali zote, akiwazuru watu nyumbani kwao, matajiri na masikini pia, wasomi na wasio wasomi, akitaka kuwafikisha juu ya mambo ya milele, wala siyo mambo hafifu tu ya dunia. Yeye hakuchafuliwa na mambo ya dunia hii walakini akapata furaha katika kuangalia mambo ya asili na viumbe vyake. Furaha ya arusi ya Wayahudi haikuwa chukizo kwake. Kule kuhudhuria kwake kwenye arusi kulikuwa kuiheshimu ndoa, kwamba ni jambo takatifu lililoanzishwa na Mungu mwenyewe.TVV 77.4

    Katika Agano la Kale na Agano Jipya pia, ndoa ni mfano wa mwungano mtakatifu ulioko baina ya Yesu na watu wake. Katika mawazo ya Yesu, furaha ya arusi ni mfano wa furaha ya siku ile ambayo kanisa la Mungu, likiwa kama bibi arusi litakapokaribishwa nyumbani mbinguni, yaani watu waliookolewa.TVV 77.5

    “Kama bwana arusi anavyomfurahia bibi arusi, ndivyo nitakavyokufurahia wewe. Atakushangilia kwa shangwe; . . . . Atakufuahia kwa kuimba.” Isaya 62:6, 7; Sefania 3:17. Yohana mtume aliandika: “Nilisikia kama sauti ya watu wengi . . . ikisema. ... Na tufurahi, tushangilie, na tumtukuze; kwa maana arusi ya Mwana-kondoo imekuja, na bibi arusi amekwisha kuwa tayari.” Ufunuo 19:6, 7.TVV 78.1

    Yesu aliwafikia watu katika roho zao kwa kuwa alijichanganya kati yao, kama mtu anayewatakia heri. Aliwatafuta popote, njiani, nyumbani, baharini, kwenye mashua, sinagogini, katika karamu ya arusi, na mahali popote. Alionyesha fadhili zake katika mambo yao yote. Huruma zake ziliwavuta kwake. Maombi yake ya pekee katika milima, yalikuwa ndiyo matayarisho kwa kazi yake ya kukutana na watu katika shughuli zao. Kutoka katika maombi hayo alikuja akiwa tayari kuwasaidia wagonjwa, na kuzivunja pingu za Shetani alizofunga watu.TVV 78.2

    Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kwa njia ya kuishi na kushirikiana nao. Wakati mwingine wakiwa kando ya mlima, wakati mwingine wakiwa pwani ya bahari, au wakiwa wanatembea njiani, hapo ndipo aliwafundisha siri ya ufalme wa Mungu. Hakuhubiri, bali alifundisha; wala hakuwaamuru wanafunzi wake wafanye hili au lile, ila alisema: “Nifuateni.” Rafiki zake alifuatana nao ili wapate kuona jinsi anavyofundisha watu.TVV 78.3

    Kielelezo cha Kristo kinapaswa kuigwa na wote wanaofundisha Neno lake. Haitupasi kujitenga na watu, bali kushirikiana na watu wa hali mbali mbali, mahali popote walipo. Roho za watu haziguswi kwa njia ya mahubiri mimbarani peke yake. Njia nyingine ya kuwafikia watu, ambayo inafaulu sana ni katika nyumba za watu wa hali ya chini, na nyumba za watu wa hali ya juu, na katika makusanyiko halali.TVV 78.4

    Haitupasi kuunganika na watu wa ulimwengu katika mambo yao ya ufedhuli. Tusiihalalishe dhambi kwa na yoyote, kwa maneno yetu, au kwa matendo yetu, au kwa kukaa kimya kwetu, au kwa kuhudhuria mahali pa dhambi. Popote tuendapo lazima twende na Yesu. Lazima tuwe mashahidi wa Yesu popote. Katika mikusanyiko yote, inayotakaswa na neema ya Yesu, lazima iwe ya kuongoa watu. Watu waone kuwa dini yetu si dini ya udhalimu bali ni ya kweli iliyojaa utu wema na baraka, hata watu watuone kuwa tunataka hata wao washiriki baraka hizo. Wote waliomwamini Kristo wawe wahudumu wa mambo mema kwa wengine, sawa kama yeye alivyokuwa mhudumu kwa watu.TVV 78.5

    Tusiupotoshe ulimwengu kwa kutudhania kuwa, Ukristo umetufanya kuwa watu hafifu wasio na faida yoyote. Watu wa Kristo hawaishi kama wenye masikitiko, wasio na furaha, watu baridi, bali wenye furaha, wachangamfu, waliojaa upendo na matendo mema, watu wa Mungu hasa. Nuru yao iwamulikie wengine kuwa na kazi njema za upendo wa Kristo.TVV 79.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents