Kuzidi kupita kiasi kwa uovu wa siku za mwisho.
Kristo aliendelea kusema: “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika, Safina, wasitambue hata Gharika ikaja ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”TVV 357.1
Siku za Nuhu zilikuwaje? “Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani, na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni haya tu siku zote,” (Mwanzo 6:5). Watu wa siku za Nuhu walifuata dhana zao ovu na mawazo yaliyopotoka. Kwa sababu ya uovu wao waliangamia. Leo ulimwengu unashika njia ile ile.Waasi wa sheria ya Mungu wanaujaza ulimwengu na maovu. Uchezaji wa kamari, ufedhuli, tamaa mbaya na ahiki zisizozuilika, yote hayo yanaujaza ulimwengu kwa maasi.TVV 357.2
Kristo alisema; “Kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema hii ya ufalme itahubiriwa katika ulimwenguni wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Kabla ya kuanguka Yerusalemu, Paulo aliishuhudia Injili “iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu,” (Wakolosai 1:23). Na sasa, injili ya milele itahubiriwa kwa “kila taifa na kabila na lugha na jamaa,” (Ufunuo 14:6). Kristo hakusema ulimwengu wote utaongolewa bali kwamba, “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, ndipo ule mwisho utakapokuja.” Kwa njia ya kuhubiri injili ulimwenguni, lutaharakisha kurudi kwake Yesu. Sisi litupasi tu kutazamia kuja kwa Yesu bali pia kuharakisha kuja kwa siku ya Mungu. (Tazama 2 Petro 3:12.) Kama kanisa lingefanya kazi liliyopewa na Bwana, ulimwengu wote ungekuwa umeonywa na Yesu angekuwa amerudi.TVV 357.3
Jambo la kuishi kwalo! Kwa kuwa hatujui wakati kamili wa kurudi kwake Bwana, tumeagizwa kukesha. (Tazama Luka 12:37.) Wale wanaokesha kwa kurudi kwa Bwana hawawezi kukesha katika hali ya uvivu. Watakuwa wakijitakasa roho zao, kwa kuitii ile kweli. Pamoja na bidii ya kukesha kutakuwepo na kufanya kazi kwa dhati. Juhudi yao itaamshwa ili kushirikiana na mbingu katika shughuli ya wokovu wa wanadamu. Wanatangaza ujumbe unaopasa kwa saa hii. Kama walivyokuwa akina Enoki, Nuhu, Ibrahimu na Musa kila mmoja alivyotangaza ujumbe kwa wakati wake, ndivyo watumishi wa Kristo watakavyolitangaza onyo maalum kwa kizazi chao.TVV 357.4
Lakini Kristo analitaja kundi jingine pia: “Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi Bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua;”TVV 358.1
Mtumishi mwovu hasemi kuwa Bwana hawezi kuja. Ila katika matendo na maneno yake hutangaza kuwa kuja kwa Bwana kunakawia. Huondoa katika mawazo ya wengine kule kumtazamia Bwana aje karibu. Mvuto wake huwathibitisha wengine katika mambo ya ulimwengu na bumbuazi. Tamaa za ulimwengu humpumbazisha na kumtawala akili. Mtumishi mwovu huwapiga watumishi wenzake, akiwashitaki na kuwashutumu wale waliowaaminifu kwa Bwana wao. Hujichanganya na walimwengu, na kwa njia hiyo hunaswa mtegoni. “Bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki.”TVV 358.2
Kurudi kwa Kristo kutawaghafdisha walimu wa uongo. Kwa wale wote wenye kuufanya ulimwengu huu kuwa makao yao siku ya Mungu itawapata kama mtego unasao, na kama mwizi ajaye usiku. Ulimwengu ukiwa umezama katika machafuko na anasa za ufedhuli, umelala katika utulivu wa mauti. Watu huyacheka maonyo; “Na kesho itakuwa kama leo, sikukuu kupita kiasi.” Isaya 56:12. Tutatazama zaidi katika ya maisha ya anasa. Lakini Kristo asema: “Naja kama mwivi.” Ufunuo 16:15. Wakati wenye dhihaka wanapoende-lea kwa kiburi wakati watafula mali wanaendelea katika kupata mali bila kujali kanuni, wakati mwanafunzi anajitahidi kutafuta kila elimu, isipokuwa Biblia, Kristo atakuja kama mwizi.TVV 358.3
Kila kitu ulimwenguni kinachemka. Dalili za nyakati zinaogofya. Roho wa Mungu anaondolewa duniani taratibu, na ajali zinafuata moja baada ya nyingine katika nchi na bahari. Kuna tufani na tetemeko, mioto, mafuriko, mauaji ya kila namna. Nami awezaye kuzisoma nyakati? Usalama uko wapi? Hakuna uhakika katika cho chote kile cha mwanadamu au ulimwengu.TVV 358.4
Wako wale wanaongojea, wakikesha na kutenda kazi kwa ajili ya kurudi kwa Bwana wetu. Kundi jingine linasimama katika mstari wa yule mwasi mkuu wa kwanza.TVV 358.5
Hatari inatujia pole pole. Jua linang’aa mbinguni, likiendelea na mzunguko wake wa kawaida juu mbi-nguni. Watu wanaendelea kula na kunywa, wakipanda na kujenga majumba. Wafanya biashara wanaendelea kuuza na kununua. Watu wanagombea madaraka. Wenye kupenda anasa wanajazana katika majumba ya starehe zao mashindano ya Farasi michezo yakamali. Ashiki kuu hutawala, na huku saa ya mlango wa rehema kufungwa inaharakisha na kila jambo karibu linakatwa kwa milele. Shetani amewaweka wakala wake wote shughulini ili wanadamu wadanganywe, na kupotoshwa, mpaka mlango wa rehema umefungwa milele.TVV 358.6
“Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.TVV 359.1