Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukoo wa utawala watoa changamoto kwa Kristo

  Madhehebu mawili, yaani Mafarisayo na Masadukayo, walikuwa maadui wakubwa sana wa Kristo. Wao walikuwa wakitaka kuona ishara kutoka mbinguni. Wakati Waisraeli walipopigana na wakanaani huko Bethhoroni, jua lilisimama wakati Yoshua alipomwomba Mungu iwe hivyo. Ishara ya aina hiyo ilitakiwa pia wakati wa Yesu, lakini hakuna ishara yoyote ingaliwafaa, kama ushahidi wa Yesu kwamba ni Masihi.TVV 227.2

  Yesu alisema: “Enyi wanafiki, mnaweza kutambua nyakati, za majira.” Kwa kuchunguza wanaweza kutabiri nyakati. “Lakini hamwezi kutambua ishara za wakati?” Maneno ya kristo yalinenwa kwa nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu, hayo ndiyo ishara iliyotolewa na Mungu, wimbo ulioimbwa na malaika kwa wachungaji, nyota iliyowaongoza mamajusi, sauti iliyotoka mbinguni wakati wa ubatizo wake, ulikuwa ushahidi kamili wa kumshuhudia Yesu kuwa ni Masihi.TVV 227.3

  Yesu akahuzunika rohoni mwake, akasema, akasema, “Kwa nini kizazi hiki chataka ishara?” “Hakitapata ishara, ila ni ile ishara ya nabii yona.” Jinsi mahubiri ya Yona yalivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, vivyo hivyo mahubiri ya Kristo yalikuwa ishara kwa kizazi chake. Lakini ni tofauti kiasi gani ya mapokeo ya neno la Mungu! Watu wa mataifa katika mji mkuu wa Ninawi walijinyenyekeza mbele za Mungu, wakubwa na wadogo walimlilia Mungu wa mbinguni wakahurumiwa.TVV 227.4

  “Watu wa Ninawi watasima siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki”, asema Yesu, “nao watawahukumu, kuwa wamekosa kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.” Mathayo 12:41.TVV 227.5

  Kila mwujiza uliofanywa na Kristo, ulikuwa ishara ya Uungu wake, lakini kwa Mafarisayo ilikuwa machukizo. Viongozi wa Wayahudi waliangalia dhiki ya watu kwa mioyo ya kutojali. Kwa hiyo katika kazi nyingi za Kristo za kuwasaidia wenye dhiki hao zilikuwa kikwazo kwao. Hivyo miujiza yote ya Yesu ya kuponya watu, kwao ilikuwa kazi bure tu.TVV 227.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents