Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    80 — Yesu Apumzika Katika Kaburi La Yusufu

    Hatimaye siku ya fedheha na mateso ilikwisha. Wakati jua lilipokuwa likikaribisha Sabato, Mwana wa Mungu alipumzika katika kaburi la Yusufu; kazi yake ikiwa imemalizika. Mwanzoni Baba na Mwana walipumzika baada ya kazi yao ya uumbaji. (Tazama Mwanzo 2: 1.) Mbingu yote ilishangilia kutafakari tukio hilo la utakatifu. Sasa Yesu alipumzika baada ya kazi ya ukombozi: ingawa duniani kulikuwa na huzuni kwa wale walionipenda, lakini mbinguni kulikuwa na shangwe kuu. Mungu na malaika waliliona taifa lililokombolewa ambalo baada ya kuishinda dhambi, kamwe wasingeweza kushindwa hii ikiwa ni matokeo yatakayotokana na kazi ya Kristo iliyokamilika.TVV 436.1

    Wakati “vitu vyote vitafanywa upya.” Mnd 3:21. Sabato ya uumbaji, siku ambayo Yesu alilala akipumzikia katika kaburi la Yusufu, bado itakuwa ni siku ya kupumzika na kufurahi. “Sabato hadi Sabato.” Isaya 66:23. Mataifa ya waliookolewa watasujudu kwa furaha kumwabudu Mungu Mwana kondoo. Katika matukio ya mwisho ya siku ya kusulibishwa ushahidi mpya juu ya Uungu wa Kristo ulitolewa. Kilio cha mwisho cha Yesu kukata roho kilipotolewa, sauti nyingine ilisikika ikisema: “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.” Mathayo 27:54. Maneno hayo hayakusemwa kwa kunong’oneza. Ni nani aliyeyasema? Ni (akida) askari wa Kirumi. Uvumilivu wa Uungu wa Mwokozi, kifo chake cha ghafula, kilio kikuu cha ushindi kilichotoka mdomoni mwake vilimthibitishia Mrumi huyu mshenzi. Katika mwili wenye majeraha uliongikwa msalabani huyu akida alimtambua Mwana wa Mungu. Katika siku ile ya kifo chake Mkombozi, watu watatu walitangaza imani yao yule aliyekuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi cha Kirumi, yule aliyebeba msalaba na yule aliyekufa kando yake. Jioni ilipokaribia hali ya kimya isiyokuwa ya kawaida ilitulia juu ya Kalivari. Watu wengi walikuwa wamekusanyika kutokana na udadisi na wala siyo kutokana na chuki kwa Yesu. Hata hivyo walimwangalia Yesu kama mkosaji. Wakiwa chini ya msisimko usio wa asili walikuwa wamejumuika katika kumdhihaki. Lakini giza lilipofunika nchi, walijisikia wenye hatia ya kosa kubwa. Giza lilipotoweka walielekea nyumbani kwao wakiwa kimya, huku wakiamini kuwa mashitaka ya makuhani yalikuwa ya uongo, kwamba Yesu hakuwa mwenye kujifanya. Majuma machache baadaye, wakatiTVV 436.2

    Petro alipohubiri siku ya Pentekoste walikuwa miongoni mwa maelfu walioongoka kumfuata Kristo.TVV 437.1

    Lakini wakuu wa Wayahudi hawakubadilika; chuki yao ilikuwa bado kupungua. Giza lililofunika nchi wakati wa kifo cha Kristo lilikuwa dogo kuliko giza lililofunika mioyo yao. Vitu vya asili visivyo na uhai vilikuwa vimeshuhudia Uungu wa Kristo. Lakini makuhani na wakuu wa Israeli hawakumjua Mwana wa Mungu. Walimwua Kristo; lakini hata katika saa ya kile kilichoonekana kama ushindi wao, walisumbuliwa na mashaka. Kutatokea nini tena? Walisikia sauti ikisema, “Imekwisha.” (Yohana 19:30). Walikuwa wamesikia tetemeko kuu la nchi, na walikuwa na hofu. Walitishika na Kristo aliyekuwa marehemu zaidi kuliko walivyomwogopa Kristo aliyekuwa hai. Walihofia jambo lo lote lile lililohusiana na kusulibishwa kwake.TVV 437.2

    Kwa hali yo yote ile wasingeacha mwili wake uwe msalabani na Sabato. Lingekuwa jambo la kuvunja utakatifu wa Sabato kuiacha miili ikiangikwa msalabani. Kwa hiyo wakitumia hili kama kisingizio, viongozi wa Kiyahudi walimwomba Pilato kwamba kifo cha waliosulibishwa kiharakishwe, na miili yao iondolewe kabla ya jua kuchwa. Kibali chake kikiwa kimetolewa, miguu ya wale wezi wawili ilivunjwa ili kuharakisha kifo chao; lakini Yesu alikuwa tayari amekwisha kufa. Askari wale jeuri, wakiwa wamepoozwa na waliyoyasikia na kuyaona juu ya Kristo, walijizuia wasivunje viungo vyake. Na hivyo sheria ya Pasaka ikatimia, “Wasisaze kitu chake cho, chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake.” Hesabu 9:12.TVV 437.3

    Makuhani na wakuu walishangaa kumkuta Kristo amekufa. Ilikuwa haijasikiwa kwamba mtu aliyesulubishwa amekufa saa sita tu baada ya kusulibishwa. Makuhani walitaka kuhakikisha kwamba Yesu amekwisha kufa kweli, kwa hiyo walimshauri askari amchome mkuki ubavuni. Kutoka katika jeraha hilo, kulichuruzika vijito viwili mbali mbali, kimoja cha damu na kingine cha maji. Yohana anaeleza: “Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli, .... Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie. Hapana mfuko wake utakaovunjwa.” Na tena andiko lingine lanenwa, “Watamtazama yeye waliomchoma.” Yohana 19:34-37.TVV 437.4

    Baada ya kufufuka kwake, makuhani walieneza habari kwamba Kristo hakufa msalabani, bali alizimia tu na baadaye alihuishwa. Kitendo cha askari wa Kirumi kili-thibitisha kuwa alikuwa amekufa hakika. Kama asingekuwa amekufa, lile jeraha la mkuki lingesababisha kifo cha mara moja.TVV 438.1

    Lakini Kristo hakufa kwa kuchomwa mkuki, au kutokana na maumivu ya msalabani. Kile kilio kilichotolewa kwa sauti tena kwa nguvu (Mathayo 27:50; Luka 23:46), wakati wa kukata roho na mchuruziko wa damu na maji vilitangaza kuwa alikuwa amekufa kutokana na kupasuka kwa moyo, uliopasuka kwa uchungu wa mawazo, akiwa ameuawa na dhambi za ulimwengu.TVV 438.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents