Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    45 — Kuonyeshwa Mbele Fumbo la Msalaba

    Hata kabla Kristo hajafanyika kuwa binadamu, aliona njia nzima atakayopitia ili kuwaokoa waliopotea. Kila aina ya kichomi kitakacho-mwumiza, kila aina ya ghasia atakayosukumiwa, kila aina ya dhiki atakayopitia vyote hivyo aliviona kabla hajakumbana navyo. Wakati huo alikuwa angali hajavua utukufu wa Enzi yake, na kujitwalia hali ya kibinadamu pamoja. Wakati huo alisema: “Tazama nimekuja, (Katika gomho la chuo nimeandikiwa,) Kufanya mapenzi yako Ee, Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam sheria yako imo moyoni mwangu.” Zaburi 40:7, 8.TVV 231.1

    Maisha yake katika ulimwengu huu yaliyojazwa na hali ya kazi ngumu, na kujinyima, yaliburudishwa na jambo hili, kwamba kwa kujitoa maisha yake hivyo atarudisha ulimwengu katika umoja na Mungu. Ingawa ni lazima ipitie kwenye ubatizo wa damu, ingawa ni lazima abebe mzigo mzima wa dhambi za ulimwengu wote, ingawa atapita katika ole usiosemeka; walakini kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, aliustahili msalaba.TVV 231.2

    Wakati ulikaribia alipowachagua wenzi wake katika kazi lazima wamwone yule wampendaye akiangikwa msalabani huko Kalwari. Karibuni atawaacha wakikabiliana na ulimwengu bila yeye kuwapo pamoja nao. Watateswa na watu wanaowachukia, ambao hawataki kuamini kwa hiyo alitamani kuwatayarisha vizuri kukabiliana na majaribu.TVV 231.3

    Sasa Yesu na wanafunzi wake walifika katika mji wa Kaisaria-Filipi. Walikuwa ng’ambo ya Galilaya, mahali umizimu ulikuwa ukistawi sana. Kuwazunguka kulikuwa na hali ya ukafiri na ushirikina unaoenea ulimwenguni pote. Yesu alitaka mambo ya namna hii yawatie moyo wa kuuhurumia ulimwengu, na kujitia kikamilifu katika kazi ya kuhudumia watu wa mataifa.TVV 231.4

    Alikuwa karibu kuwaeleza kuhusu mateso yanayomkabili. Lanili kwanza aliwaombea ili mioyo yao iweze kuyapokea maneno hayo. Hakuanza kuwaeleza mambo hayo mara moja, ila aliwapa nafasi kwanza ya kuthibitisha imani yao kwake. Kea hiyo aliwauliza akisema: “Watu huninenaje mimi, Mwana wa Adamu, kwamba ni nani?”TVV 232.1

    Wanafunzi walisema kwa masikitiko kuwa Waisraeli wameshindwa kumtambua Masihi. Makutano huko Bethsaida walitamani wamtawaze awe mfalme wa Israeli. Watu wengi walikuwa tayari kumkubali kwamba ni nabii, lakini hawakumkubali kwamba ni Masihi.TVV 232.2

    Sasa Yesu aliuliza swali la pili, linalowahusu wao: “Na ninyi huninena mimi kuwa ni nani?” Petro alijibu, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.”TVV 232.3

    Tangu mwanzo Petro alikuwa amemwamini Yesu kuwa ni Masihi. Wengi wa waliomwamini yesu kuwa ni Masihi. Wengi wa waliomwamini walianza kuwa na mashaka kwa kazi ya Yohana Mbatizaji wakati alipotiwa gerezani, na kuhukumiwa kifo. Wakawa na mashaka kuwa yesu siye masihi. Wengi waliomdhania kuwa atatawala katika kiti cha Daudi, walianza kuondoka walipoona kuwa hana kusudi hilo. Lakini kusitasita kwa wale waliokuwa wakitangatanga hakukuweza kuharibu imani ya watu wa kweli. Petro alitamka: “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.” Hakungojea mpaka atawazwe kwanza, ila alimwamini katika unyenyekevu wake.TVV 232.4

    Petro alikuwa ameeleza imani badala ya wanafunzi wote, kwamba wanamkiri Yesu kuwa ndiye Masihi. Walakini upinzani wa Makuhani na wakuu wa Kiyahudi uliwapa wasiwasi sana. Hata hawakujua mahali pa kuendea. Mafundisho waliyofundishwa na Marabi hapo kwanza, na msisitizo wa kufuata mapokeo vilipingana na ukweli. Nuru ya kweli ilikuwa imeng’aa mioyoni mwao walakini walifanana kama watu wanaopapasa-papasa gizani. Lakini siku hiyo Roho Mtakatifu aliwavuvia mioyoni mwao. Badala ya kubahatisha kibinadamu, walifunuliwa dhahiri na utukufu wa Mwana wa Mungu.TVV 232.5

    Yesu alimjibu Petro akisema: “Heri wewe simon Bar Yona; maana mwili na damu havikukufunulia, ila Baba yangu aliye mbinguni.”TVV 232.6

    Ukweli uliosemwa na petro ndio msingi wa imani ya kila mwongofu. Lakini hakufunuliwa kwa ajili ya hekima yake, wala wema wake. Kwa kuwa Petro alitambua utukufu wa kristo, hilo lilithibitisha kuwa amefundishwa na Mungu. Soma Zaburi 25:14; Yohana 6:45.TVV 232.7

    Yesu aliendelea kusema: “Nakuambia tena, wewe ndiwe Petro, na juu ya Mwamba huu, nitalijenga kanisa langu, na milango ya kuzimu haitalishmda.” Neno Petro linamaanisha ji we linalovingirika. Petro hakuwa Mwamba ambao Yesu atajenga kanisa lake. Milango ya kuzimu ilimshinda wakati alipomkana Bwana wake kwa kulaani na kuapa. Kanisa lilijengwa kwa yule ambaye milango ya kuzimu haikumshinda.TVV 233.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents