Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Sala ya Kristo Ilivyojibiwa

    Maumivu ya moyo ya Kristo hayakukoma, ila unyong’onyevu na kukata tamaa vilimtoka. Dhoruba haikuwa imekoma lakini alitiwa nguvu ili kukabili ghadhabu yake. Amani ya mbinguni ilitua juu ya uso wake uliokuwa na damu. Amestahimili mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyastahimili; maana alionja mauniivu ya kifo kimpasacho kila mtu.TVV 390.2

    Wanafunzi waliokuwa wamelala waligutuka, kwa ghafula, wakamwona malaika. Wakamsikia akimwambia Mwokozi maneno ya faraja na tumaini. Sasa hawakuwa na hofu tena kwa ajili ya Bwana wao; maana alikuwa katika ulinzi wa Mungu. Mara nyingine tena wanafunzi wakashindwa na uzito wa usingizi na kwa mara nyingine tena Yesu akawakuta wamelala.TVV 390.3

    Yesu akiwatazama kwa masikitiko akasema: “Laleni sasa, mpumzike; yatosha, saa imekuja tazama, na Mwana wa Adamu sasa anatiwa mikononi mwao wenye dhambi.” Hata alipokuwa akisema hayo, alisikia vishindo kundi kubwa likimtafuta, na akasema, “Ondokeni, twende zetu; tazama yule anayenisaliti amekaribia.”TVV 390.4

    Huzuni na maumivu yaliyokuwako kwa Yesu havikuonekana tena, wakati akienda kukutana na msaliti wake. “Ni nani mnayemtafuta? Wao wakamjibu: “Ni Yesu Mnazareti.”TVV 390.5

    Yesu akawajibu “Ni mimi.” Aliposema hivyo, malaika aliyekuwa akimhudumia Yesu alipita kati ya kundi hilo na Yesu. Nuru ya uungu ikaangaza uso wa Mwokozi. Mbele ya utukufu huu kutoka mbinguni, hili kundi la wauaji wenye ghasia, likapepesuka kurudi nyuma. Hata Yuda naye akaaanguka chini.TVV 390.6

    Malaika akatoweka, na ile nuru ikafifilia mbali. Yesu alikuwa na nafasi ya kutoroka lakini aliendelea kubakia pale pale kati ya wakaidi hao, waliokuwa wakigaagaa chini bila msaada.TVV 390.7

    Mara moja mambo yalibadilika. Askari wa Kirumi, makuhani, pamoja na Yuda walimzunguka Yesu, wakiwa na wasiwasi kwamba atatoroka. Walikuwa wamepata ushahidi wa kutosha kuwa aliyesimama mbele zao alikuwa Mwana wa Mungu, lakini hawakutaka kusadiki. Kuhusu swali la kuwa “Ni nani mnayemtafuta?” Tena wakajibu, “Yesu Mnazareti.” Ndipo Mwokozi akasema “Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi waacheni hawa waende zao,” akiwasonda wanafunzi. Kwa ajili yao alikuwa tayari kujitoa mhanga.TVV 391.1

    Yuda msaliti hakusahau sehemu yake. Alikuwa amewapa ishara waliokuwa wanamtafuta Yesu, akisema, “Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni mkamchukue salama.” Sasa, akimkaribia Yesu alimshika mkono kama rafiki akisema: “Salamu Rabi, akambusu mara kadhaa, na alionekana kana kwamba analia kwa kumsikitikia katika hatari yake.TVV 391.2

    Yesu akasema: “Rafiki, fanya ulilolijia.” Huku sauti yake ikitetemeka kwa huzuni, akaongeza, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?” Maneno haya yalipasa kugusa dhamiri ya msaliti, lakini heshima na huruma ya kibinadamu vilikuwa vimemtoka. Alikuwa amejitolea kwa Shetani, na hakuwa na uwezo wa kumpinga. Yesu hakukataa busu ya msaliti.TVV 391.3

    Lile kundi la watu sasa likamkamata Yesu, na kuanza kuifunga mikono ile iliyokuwa ikitumika katika kutenda mema.TVV 391.4

    Wanafunzi walikatishwa tamaa na kukasirishwa walipoona kamba zikitolewa kufunga mikono ya yule waliyempenda. Petro kwa hasira akatoa upanga na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani Mkuu. Yesu alipoona haya aliondoa mikono yake ingawa ilishikiliwa na askari wa Kirumi kwa nguvu, akasema: “Mwe radhi kwa hili.” Akamgusa sikio akamponya mara moja.TVV 391.5

    Kisha akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako mahali pake; maana wote waushikao upanga wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?” Jeshi badala ya kila mwanafunzi. Aa, Kwa nini, wanafunzi wake walifikiri hajiokoi nafsi yake na sisi? Akijibu mawazo yao akaongeza, “Yatatimizwaje maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?” Je! kikombe alichonipa Baba mimi nisikinywee?”TVV 391.6

    Makuhani wadanganyifu na wazee walikuwa wamefuatana na polisi wa hekalu na kundi la watu wakipiga makelele katika kumfuata Yuda mpaka Gethsemane. Hawa waheshimiwa walifuatana kundi la ajabu kiasi gani kundi lililojivika silaha, kana kwamba linafukuza mnyama wa porini!TVV 392.1

    Kristo akiwageukia makuhani na wazee, alisema maneno ambayo hawatayasahau kamwe; “Je, mmetoka kama kumkamata mnyang’anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku naliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.” Usiku ndio unaowafaa mfanye kazi yenu. Lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.”TVV 392.2

    Wanafunzi walishikwa na hofu walipoona Yesu anajiruhusu kukamatwa na kufungwa. Walichukizwa kwamba anadhalilishwa hivyo pamoja na wao. Ha-wakuweza kuelewa huu msimamo wake, na wakamlaumu kwa kujisalimisha. Katika ghadhabu na woga wao, Petro akapendekeza wajiokoe wenyewe. Wakikubaliana na wazo hilo, “wote wakamwacha, wakakimbia.”TVV 392.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents