Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kayafa Ahimiza Udanganyifu

    Kayafa alijaribu kusema jambo. Midomo ilitikisika, lakini bila neno kutoka. Askari walikuwa tayari kutoka kwenda zao, ndipo Kayafa akasema. Ngojeni, ngojeni kwanza. Msimwambie mtu ye yote mliyoona.TVV 442.1

    Makuhani wakasema: “Semeni ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipo kuwa tumelala.” Hapa makuhani walivuka mpaka. Maana kama walikuwa wamelala watajuaje? Na kama wanafunzi walikuwa na hatia ya kuuiba mwili wa Kristo, makuhani wasingalikuwa wa kwanza kuwahukumu? Au kama walinzi walilala, makuhani wasingaliwachukulia na kuwashitaki kwa Pilato?TVV 442.2

    Askari waliogopa sana. Kulala katika zamu lilikuwa kosa baya listahililo hukumu ya kifo. Je, watakubali kushuhudia uongo, na kujiweka katika hatari ya kufa? Je, watawezaje kukabili hata kama ni kwa kulipwa fedha ikiwa wanajishuhudia uongo wenyewe?TVV 442.3

    Makuhani waliahidi kuwalinda askari walinzi hawa, wakisema kuwa Pilato hatataka kusikia habari hizo zikienea kama wao wasivyotaka. Askari wa Kirumi waliuliza uaminifu wao kwa fedha. Walikuja kwa makuhani wakiwa na mzigo wa habari za ukweli wa kushtusha; wakaondoka kurudi wakiwa na mzigo wa fedha, na katika vinywa vyao taarifa ya uongo.TVV 442.4

    Wakati huo habari za kufufuka kwake Yesu zilikuwa zimefika kwa Pilato. Ingawa alimhukumu Mwokozi bila kutaka, hakuwa na majuto yo yote mpaka sasa. Kwa hofu sasa alijifungia nyumbani mwake, wala hakutaka kuonana na mtu. Lakini makuhani walikwenda kwake, wakamsihi asijali habari za walinzi kutoangalia kazi yao. Yeye mwenyewe aliwauliza walinzi kwa siri, wala hawakumficha neno lo lote, na Pilato alielezwa yote yaliyotokea. Hakuyajali, wala kuyashughulikia mambo hayo, lakini tangu siku hiyo hapakuwa na amani kwake.TVV 442.5

    Makuhani kwa kumwua Kristo, walijifanya kuwa vyombo vya Shetani. Sasa walikuwa watu wake kamili, wakiwa wamenaswa katika mtego ambao hawakuweza kujinasua, ila tu kuendelea na vita vyao juu ya Kristo. Usalama wao ni kuonyesha kuwa Kristo ni laghai kwa kukanusha kuwa hakufufuka. Hivyo waliwahonga askari na kumfanya Pilato akae kimya.TVV 442.6

    Lakini palikuwapo mashahidi wasioweza kuwa nyamazisha. Wengi walikuwa wamesikia ushuhuda wa askari kuhusu kufufuka kwa Kristo. Na hakika ya wafu waliofufuka pamoja na Kristo, walionekana na wengi na kutangaza kuwa Kristo amefufuka. Makuhani na wakuu walikuwa wakihofu daima kuwa siku moja wanaweza kukutana na Kristo mwenyewe njiani. Makufuli na vyuma vilivyowekwa milangoni havikuweza kumzuia Mwana wa Mungu. Daima mchana na usiku lile tukio la kutisha wakati walipopaza sauti kwamba: “Damu yake iwe u yetu na juu ya watoto wetu.” Mathayo 27:25. Lilikuwa mbele zao.TVV 443.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents