Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kristo asingeweza kununuliwa

    Wakati mjaribu alipotoa ufalme wa ulimwengu kwa hari zake, alikusudia kuwa Kristo ashikiliwe chini ya Shetani. Huu ulikuwa ufalme ule ambao ulitumainiwa na Wayahudi. Wao walitamani ufalme wa dunia hii. Lakini Kristo alimwambia mjarilbu. “Nenda nyuma yangu, Shetani: maana imeandikwa, “Utamsujudia Bwana Mungu wako, yeye peke yake utamwabudu.” Kristo asingeweza kununuliwa. Amekuja kusimamisha ufalme wa haki, naye asingeliacha kutimiza kusudi lake.TVV 64.1

    Shetani huwafikia watu akiwajaribu na jaribu hilo hilo, naye hufaulu sana kuliko kwa Kristo. Huwapa ufalme wa dunia hii kwa sharti moja, yaani wauache unyofu wao kwa Mungu, na kuukiri ukuu wa Shetani. Husema, chochote cha kuendesha maisha haya yawe na mafanikio, kifanye, ndiko kunitumikia. Mimi nitawapa utajiri, anasa, heshima, na furaha. Msichukuliwe na hali ya unyofu na kujikana nafsi.TVV 64.2

    Hivyo makundi ya watu hupendelea maisha ya anasa na ubinafsi, na Shetani huridhika. Lakini huwapa kitu ambacho sicho chake, ambacho kitatoweka mara. Badala yake huwapotosha wakaacha haki ya kurithi na kuwa wana wa Mungu.TVV 64.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents