Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuridhia Kwaelekeza Katika Maangamizi

    Wakati Pilato alipomtoa Yesu ili apigwe mijeledi alitegemea kuwa ule umati utaamua kuwa adhabu hiyo imetosha. Lakini kwa makini sana Wayahudi waliona udhaifu wa kumwadhibu mtu aliyekuwa ametamkwa kuwa hana hatia, walidhamiria kuona kuwa Yesu haachiliwi.TVV 416.1

    Pilato sasa aliagiza baraba aletwe mahakamani, na wafungwa wote wawili wakasimama pamoja. Akimsonda Mwokozi kwa kidole akasema “Tazama mtu huyu!” Hapo alisimama Mwana wa Mungu, amefungwa nguo kiunoni tu, mgongo wake ukionyesha majeraha yadamu, umevimba na ukionyesha maumivu, lakini ulikuwa haujapata kupendeza hivyo. Kila sehemu ya uso ilidhihirisha huruma ya upole kwa maadui zake wakatili. Katika jinsi yake kulikuwa na nguvu na heshima ya uvumilivu. Alikuwa tofauti na mfungwa mwenzake aliyesimama pamoja naye. Kila mshipa wa uso wa Baraba ulimtangaza kuwa jambazi sugu. Tofauti kati yao ilikuwa dhahiri kwa kila mtu aliyewaona. Baadhi ya waliomwangalia Yesu walilia mioyo yao ikiwa imejaa huruma. Makuhani na wakuu walisadikishwa kuwa alivyokuwa akidai ndivyo alivyokuwa.TVV 416.2

    Askari wa Kirumi waliomzunguka Yesu hawakuwa wakaidi wote. Walimtazama mteswa kutoka mbinguni kwa masikitiko na huruma, uvumilivu wake mtulivu uliwagusa mioyo yao. Maono haya kamwe hayatawatoka mpaka ama wamkiri yeye kuwa Kristo au kwa kumkataa wajikatie hukumu wao wenyewe.TVV 416.3

    Pilato hakuwa na mashaka kuwa hali tofauti ya Mtu huyu na Baraba itawagusa Wayahudi wawe na huruma. Lakini hakufahamu ushupavu wa chuki ya Makuhani. Kwa mara nyingine tena, makuhani, wakuu na watu walipiga kelele cha kutisha: “Asulibishwe, Asulibishwe.” Mwishowe Pilato akiwa ameshindwa kuvumilia ukatili wao usiokuwa na maana alipaza sauti kwa kukata tamaa: “Mtwaeni ninyi basi, mkamsulubishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake.”TVV 416.4

    Gavana wa Kirumi, ingawa alizoea kuona matukio ya ukatili, alimwonea huruma mfungwa huyu mteswa. Lakini makuhani walipiga kelele, “Sisi tunayo sheria na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu.”TVV 416.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents