Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Kristo anavyo safisha moyo kutokana na dhambi

  Kazi ya Kristo ya kumtakasa mwenye ukoma ni kielelezo cha jinsi anavyosafisha moyo wenye dhambi. Mtu yule aliyemjia Kristo alikuwa amejaa “ukoma mwili mzima.” Wanafunzi walitaka kumzuia Mwalimu wao asimguse. Lakini alipomwekea mikono yake kwenye ukoma, hakunajisika. Kule kumgusa kulileta uwezo wa kupona.TVV 143.3

  Hivyo ndivyo ilivyo kwa ukoma wa dhambi. Haiwezekani kuponyesha kwa uwezo wa kibinadamu. Kutoka katika nyayo za miguu mpaka kichwani, hakuna uzima, ila ni vidonda, na majeraha, yatokayo usaha.” Isaya 1:6. Lakini Yesu anao uwezo wa kuponya. Mtu yeyote atakayeanguka miguuni mwake na kusema”, kwa imani, “Bwana ukitaka waweza kuni takasa”, ataweza kusikia jibu, “Nataka takasika.”TVV 143.4

  Nyakati nyingine, Yesu hakutoa uwezo wa kuponya mara moja. Katika habari za mwenye ukoma huyu, ombi lake lilishughulikiwa mara moja.TVV 143.5

  Tunapoomba vitu vya dunia jawabu pengine hutupatia kitu kingine badala ya kile tulichoomba. Lakini haitakuwa hivyo tunapoomba kuokolewa, kutokana na dhambi. Ni mapenzi yake kututakasa na kutufanya wana wake kamili, tuishi bila dhambi. Kristo alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na maovu yaliyomo duniani, kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu Baba yetu. Wagalatia 1:4. Tukiomba kitu kwa kadiri ya mapenzi yake atusikia. Na tukijua kuwa atusikia, kwa yote tuombayo, hujua ya kuwa tunayapokea yale tuombayo. Yohana 5:14, 15.TVV 144.1

  Katika kumponya mtu aliye huko Kapernaumu, Kristo alifundisha fundisho lile lile tena., Alidhihirisha uwezo wake wa kusamehe dhambi, ndipo alipofaya mwujiza. Sawa na mwenye ukoma, huyo wa kupooza naye hakuwa na tumaini lolote. Ugonjwa wake ulisababishwa na maisha yake mabaya. Na ugonjwa wake ulikuwa wa kuchukiza sana. Alikuwa amewataka Mafarisayo na waganga, lakini hawakuweza kumponya, walimwacha tu katika masumbuko yake.TVV 144.2

  Alipoona kuwa hakuna tumaini lolote mahali popote alikata tamaa kabisa. Kisha alisikia habari za Yesu. Rafiki zake walimtia moyo kuwa kama akimwendea Yesu kwa imani ataweza kuponywa. Watamchukua na kumpeleka kwake.TVV 144.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents