Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fundisho la Sabato

    Sabato moja Yesu na wanafunzi wake walipopita katika shamba la nafaka iliyoiva, wanafunzi walianza kuvunja masuke yake, na kuyapukuchua na kuyala. Katika siku nyingine ya juma jambo hili lisingekuwa kitu, maana ilikuwa kawaida kwa mtu yeyote anayepita katika shamba la matunda au shamba la ngano kula kitu cho chote atakacho. Soma Torati 23:23, 25. Lakini kufanya hivyo siku ya Sabato ilikuwa haramu. Kupukuchua masuke ilihesabika kama kuvuna au kupura.TVV 153.4

    Wapelelezi mara moja walilalamika kwa Yesu wakisema: “Tazama wanafunzi wako wanatenda tendo lisilo halali kutenda siku ya Sabato.” Marko 2:24.TVV 154.1

    Wakati Yesu aliposhitakiwa huko Bethesda kuwa amevunja Sabato, alijitetea kwa kujithibitishia kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, akisema kuwa anatenda kazi kufuatana na mapenzi ya Mungu. Na sasa kwa kuwa wanafunzi wake wameshambuliwa, alitaja mfano katika Agano la Kale, katika siku ya Sabato wakati wale waliokuwa wakihudumu mbele za Mungu. Katika majibu ya Mwokozi, aliwakemea kwa kutojua maandiko: “Hamjasoma jinsi Daudi alivyofanya alipokuwa na njaa yeye na wale aliokuwa nao, jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu akatwaa mikate ya onyesho akala, ambayo si halali kwa mtu yeyote kuila isipokuwa kwa makuhani pake yao?” Akawaambia, Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya Sabato.” Au hamjasoma katika sheria jinsi makuhani walivyo najinsi Sabato na wanajiona kuwa hawana hatia?” Nawaambia kuwa kitu kikuu zaidi kuliko hekalu. “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” Luka 6:3, 4; Marko 2:27, 28; Mathayo 12:5, 6, 8.TVV 154.2

    Kama ilikuwa haki kwa Daudi kula mikate iliyotengwa kwa ajili ya matumizi matakatifu, ilikuwa haki pia kwa wanafunzi kuvunja masuke ya ngano na kuyala siku ya Sabato. Makuhani pia walitenda kazi kubwa sana hekalu siku ya Sabato, kuliko siku nyingine. Kazi ya aina hiyo ikihusu biashara huwa dhambi, lakini walikuwa wakitenda mambo yanayohusu uwezo wa kuokoa Wakaristo, kwa hiyo kazi yao iliafikiana na Sabato.TVV 154.3

    Kusudi la kazi ya Mungu ulimwenguni ni kumwokoa mwanadamu. Kwa hiyo kitu ambacho kingefanywa kuhusiana na kazi hiyo ya ukombozi, kinapatana na sheria ya Mungu, na Sabato, wala si uvunjaji wa Sabato. Hivyo Yesu alikomesha majadiliano hayo kwa kutangaza kwamba, yeye ndiye “Bwana wa Sabato”, yaani ndiye aliye juu ya yote na juu ya sheria. Mhukumu Mkuu huyu aliwaondolea wanafunzi lawama, kwamba wamevunja Sabato.TVV 154.4

    Yesu alisema kuwa, katika upofu wao, adui zake walikosea kujua makusudi ya Sabato. Yesu alisema: “Kama mngejua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, msingemhesabia makosa, mtu asiyekuwa na makosa.” Mathayo 12:7. Dini yao ya mfano tu, haiwezi kuleta uchaji kamili na upendo wa kweli, ambao huwa katika tabia za wenye kumwabudu Mungu kikweli.TVV 154.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents