Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu Ajaribu Kumwokoa Pilato

    Yesu hakumwacha Pilato bila nuru zaidi, alimweleza kuwa Yeye hakuwa anatafuta ufalme wa dunia hii. Akasema: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. Basi Pilato akamwambia, Wewe mfalme basi? Yesu akajibu Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwengini, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.” Kristo alitamani Pilato aelewe kuwa ni kwa njia ya kuiamini kweli na kujitwalia hiyo kweli ndipo hali yake ya asili iliyohaaribiwa ingeweza kujengwa upya.TVV 410.6

    Pilato alichanganyikiwa mawazo. Moyo wake ulitamani mno upate kuijua hiyo kweli, na jinsi ya kuipata. Aliuliza: “Kweli ni nini?” Lakini hakungoja kujibiwa. Makuhani walipiga makelele wakitaka hukumu itekelezwe mara moja, alipotoka nje kwa Wayahudi alisema kwa dhati, “Mimi sioni hatia yo yote kwake.”TVV 411.1

    Makuhani na wakuu waliposikia hivyo kutoka kwa Pilato walikatishwa tamaa na kupandwa na hasira isiyo na kikomo. Walipoona uwezekano wa kuachiwa yesu, walitaka kumpasua vipande vipande. Walimlaumu Pilato, na kumshutumu kuwa hana uaminifu kwa Serikali ya Warumi. Walimlaumu kwa kutomhukumu Yesu, waliyethibitisha, alikuwa amejiinua kinyume na Kaisari. Walisema kwa hasira kuwa uchochezi wa Yesu dhidi ya Serikali ulikuwa unajulikana katika nchi yote. Wakasema: “Huwalaharisha watu, akifundisha katika Uyahudi wote, tokea Galilaya mpaka huku.”TVV 411.2

    Wakati huo Pilato hakuwa na wazo lo lote la kumtia Yesu hatiani. Alijua kuwa Wayahudi walimshitaki kwa fitina na chuki. Haki ilisema kuwa Yesu afunguliwe. Lakini kama akikataa kumtia Yesu hatiani, watu wangefanya fujo kubwa, na hili ndilo aliloogopa. Aliposikia kuwa Yesu anatoka Galilaya, aliamua kumpeleka kwa Herode, ambaye ndiye alikuwa mtawala wa huko, ambaye kwa wakati huo alikuwa Yerusalemu. Kwa njia hiyo Pilato alitaka kumtupia jukumu hilo Herode. Na ndivyo ilivyotokea. Mahakimu hawa wawili walipatana kutokana na kesi dhidi ya Mwokozi.TVV 411.3

    Katika ghasia na fujo zilizofuata Yesu aliharakishwa kwenda kwa Herode. “Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye.” Herode huyu ndiye yule ambaye mikono yake ilikuwa na damu ya Yohana Mbatizaji. Herode aliposikia habari za Yesu kwa mara ya kwanza aliogopa sana na kusema: “Yohana Mbatizaji amefufuka, katika wafu ....” Hata hivyo alitamani kumwona Yesu. Sasa nafasi ilipatikana ya kumwokoa nabii huyu, na mfalme alitamani kufutilia mbali kumbukumbu ya kichwa chenye damu kilicholetwa kwake juu ya sahani kubwa. Pia aliona kuwa ni nafasi ya kutosheleza shauku yake, na alidhani kuwa ikiwa Kristo angepewa uwezekano wa kuachiwa angeweza kutenda cho chote atakachoombwa.TVV 411.4

    Mwokozi alipoletwa, makuhani na wazee walihimiza mashitaka yao dhidi yake. Lakini Herode aliamuru kuwe kimya. Aliamuru zile pingu Kristo alizofungwa mikononi zifunguliwe, wakati ule ule akiwakemea adui zake kwa vile walivyomtendea Yesu kikatili hivi. Na yeye kama Pilato pia aliridhika kuwa Kristo ameshitakiwa kwa husuda na wivu tu.TVV 412.1

    Herode alimwuliza Kristo maneno mengi, lakini Mwokozi alinyamaza kimya tu. Kwa amri ya mfalme aliamuru wadhaifu na vilema waliletwa, na Kristo akaamuriwa athibitishe madai yake kwa kufanya muujiza. Yesu hakuitikia jambo hilo na herode alizidi kusisitiza: tuonyeshe ishara inayothibitisha usemi unaoenea kuwa unao uwezo kweli.” Lakini Mwana wa Mungu alikuwa amechukua asili ya kibinadamu, kwa hiyo inampasa kutenda kama mwanadamu katika hali kama hiyo. Hivyo hawezi kutenda miujiza ili ajiokoe kutokana na apitie maumivu na kudharauliwa ambako mwanadamu hupitia akiwa katika hali kama hii.TVV 412.2

    Herode alimwahidi yesu kuwa kama akifanya miujiza fulani, atamwachilia. Hofu iliwashika washtaki wa Kristo maana asije akafanya muujiza sasa, kitendo kama hicho kitaangamiza mipango yao kabisa, na labda kitawagarimu hata wao maisha yao pia. Makuhani na wakuu walipaza sauti zao wakasema kwamba yeye ni haini: na mkufuru; hutenda miujiza yake kwa uwezo wa mkuu wa mashetani!TVV 412.3

    Sasa dhamira ya Herode haikumsumbua sana kama alivyokuwa alipotishika na kutetemeka kutokana na ombi la Herodias kutaka kichwa cha Yohana Mbatizaji, hali yake ya kiroho ilikuwa pungufu kutokana na maisha yake ya uasherati. Hata alijivuna kwa ile adhabu aliyoitoa kwa Yohana Mbatizaji kwa kuthubutu kumkaripia. Na sasa alimtisha Yesu kuwa anao uwezo wa kumhukumu. Lakini Yesu hakuonyesha dalili yo yote, kuwa amesikia neno lo lote.TVV 412.4

    Herode aliudhika kwa ukimya huu. Ilionekana kana kwamba madaraka yake yalidharaulika. Tena kwa mara nyingine akamtishia Yesu kwa hasira lakini yeye alibakia kimya na bila kutishika duni. Kazi ya Kristo haikuwa kuridhisha shauku. Kama angalitamka neno la kuponya roho zilizolemewa na dhambi, asingalikaa kimya. Lakini hakuwa na neno kwa wale wanaoukanyaga ukweli chini ya miguu yao. Herode alikuwa amekataa ujumbe uliosemwa kwake na nabii mkuu kuliko wote, na hivyo hakukuwa na ujumbe mwingine tena. Mkuu wa mbinguni hakuwa na neno kwake. Midomo ile ilikuwa imefungwa kwa mfalme jeuri ambaye hakuhitaji Mwokozi.TVV 412.5

    Uso wa Herode ulibadilika kuwa mwepesi kwa hamaki Kwa ghadhabu, akamwita Yesu kuwa laghai, Kisha akamwambia Kristo, ikiwa huonyeshi ushahidi wo wole wa dai lako, nitakukabidhi mikononi mwa askari na watu Ikiwa wewe ni laghai, adhabu ya kifo ndiyo unayostahili, ikiwa u Mwana wa Mungu, jiokoe nafsi yako kwa kufanya muujiza. Mara maneno haya yaliposemwa adui zake walimrukia kwa kasi sana, kama wanyama. Yesu alikokotwa huko na huko, Herode akiungana nao katika kumdhalilisha Mwana wa Mungu. Kama askari wa Kirumi wasingeingilia kati, Mwokozi angepasuliwa vipande vipande.TVV 413.1

    “Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri;” askari wa Kirumi pia walijiunga katika dhihaka hii. Yale yote ambayo askari hawa wapotovu na viongozi wa Kiyahudi waliyoweza kuchochea alipakiwa Mwokozi. Hata hivyo uvumilivu wake haukutetereka.TVV 413.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents