Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Yesu alitegemea uwezo wa Baba

  Yesu aliyakanusha malaumu kuwa, anakufuru. Alisema: “Mamlaka yangu kuwa mimi Mwana wa Mungu; ambaye kwa hali niko pamoja na ninyi, yaani ninafanana na ninyi. Ninashiriki pamoja na Mungu. Mwana hawezi kufanya kitu kwa mapenzi yake mwenyewe, ila kwa yale aliyoona kwa Baba.” makuhani na Marabi walikuwa wakizungumza, Mwana wa Mungu kufanya kazi aliyotumwa na kufanya ulimwenguni. Basi kwa mambo hayo waliona kuwa wana ushahidi wa kutosha, wala hawana haja zaidi. Lakini Mwana wa Mungu alikuwa anamtegemea Baba katika uwezo wake, na hekima yake. Kristo hakujitungia mambo. Kila siku Baba alikuwa anampangia mambo. Sisi pia inatupasa tumtegemee Mungu, ili maisha yetu yapatane na mapenzi ya Mungu.TVV 111.4

  Maneno ya Kristo hutufundisha kwamba, sisi tusingejitenga mbali na Mungu, aliye Baba yetu katika mambo yetu yote, hata kama ni jambo gani, lazima tumtegemee Mungu tu. Yeye ametuweka katika kazi yoyote ile, na anatukubali kuifanya. Kadiri tunavyojitoa kwake na kuomba hekima kwake, na kumtegemea kabisa, tutaongozwa katika mapito ya usalama, na kutimiza kazi ile tuliyopewa. Lakini mtu yeyote anayejitegemea kwa akili zake, hutengana na Mungu na kusimama upande wa adui wa Mungu.TVV 112.1

  Masadukayo waliamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, lakini Yesu aliwaambia kuwa, kazi kubwa ya Baba yake ni kuamsha watu waliokufa. Na yeye mwenyewe anao uwezo wa kufanya hivyo pia. “Jinsi Baba awafufuavyo wafu, na kuwafanya waishi, vivyo hivyo na Mwana vile vile, kwa wale anaotaka. “Saa inakuja, na saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu nao watatoka.” Kristo alisema kuwa uwezo wenye kufufua wafu ulikuwa kati yao, nao wangeutazama jinsi ulivyo. Uwezo ule ule huwapa watu uzima na kuwaweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. Warumi 8:2. Kwa njia ya imani mtu hulindwa kutoka dhambini. Yeyote afunguaye moyo wake kwa Kristo, huwa mshiriki wa uwezo huo ambao utamfufua toka kaburini.TVV 112.2

  Mnazareti mnyenyekevu aliinuka juu ya wanadamu, akaitupilia mbali sura ya dhambi na aibu, akasimama ameonekana kuwa Mwana wa Mungu, ambaye ni umoja na Mungu. Mwumbaji wa ulimwengu. Wasikilizaji wake walipagawa kwa utamu wa maneno. Hakuna mtu hata mmoja aliyesema maneno kama Yeye au kuonekana kifahari kama Yeye. Matamshi yake yalikuwa dhahiri na wazi kabisa. “Baba hamhukumu mtu yeyote, lakini amekabidhi hukumu yote kwa mwana . . . Baba . . . amempa Mwana mamlaka ya kuhukumu, kwa sababu Yeye ni Mwana wa Adamu.”TVV 112.3

  Makuhani na wakuu wa watu walijifanya ndio waamuzi wa kazi ya Kristo, lakini Kristo alijitangaza mwenyewe kuwa ndiye mwamuzi wao na wa nchi yote. Kutoka kwa Mungu mafanikio yote ya watu huwajia kwa njia ya Kristo. Kwa kadiri dhambi inapokuwapo, huwapo Mwokozi pia. Aliyetoa mwanga kuwamulikia watu, ndiye anayewatafuta watu watoke dhambini waje katika utakatifu, na ndiye atayekuwa Hakimu wa wote. Yule ambaye amewasihi watu kwa vizazi na vizazi watoke katika utumwa wa dhambi, ndiye atakayewahukumu, watu wote.TVV 112.4

  Kwa kuwa Yeye ameyaonja. mavurugiko na majaribu ya wanadamu, na kufahamu dhiki ya wanadamu, na kwa kuwa aliyashinda majaribu ya Shetani, atawatendea watu mambo ya haki. Maana amewanunua kwa damu yake mwenyewe. Kwa ajili hii Mwana wa Adamu amewekwa awe Mhukumu wao.TVV 113.1

  Lakini “Mungu hakumtuma Mwanawe ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe kwa njia yake Yeye.” Yohana 3:17. Katika Sanhedrin, Yesu alisema: “Yeye alisikiaye neno langu, na kumwamini aliyenituma, anao uzima wa milele, wala haji hukumuni, bali amepita toka mauti hata uzima wa milele.”TVV 113.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents