Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wengine walitetemeka Mbele ya Yesu

  Lakini walikuwapo wengine waliotetemeka mbele ya Kristo. Wengine waliokuja kumdhihaki walirudi nyuma, wakiogopa na kunyamaza. Herode alikirishwa. Miali ya nuru ya mwisho ya rehema kwake, ilimulika moyo wake uliofanywa kuwa mgumu na dhambi. Uungu ulikuwa umeng’aa ndani ya ubinadamu. Herode aliona kuwa alikuwa akimwangalia Mungu katika kiti chake cha enzi. Katika hali yake ya ukaidi, hakuthubutu kuidhinisha hudumu dhidi ya Kristo. Alimrudisha Yesu tena katika jumba la hukumu la Kirumi.TVV 413.3

  Pilato alisikitika sana alipowaona Wayahudi wanarudi kwake wakiwa na mshitakiwa. Aliwakumbusha kuwa alikwisha kumhoji Yesu na kumkuta hana hatia yo yote ile. Mashitaka yao yote yalikuwa hayana ushahidi. Hata Herode pia ambaye ni mtu wa taifa lao, hakuona kosa lo lote lililostahili kifo. “Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua.” Hapo Pilato alionyesha udhaifu wake. Yesu hakuwa na kosa lo lote, lakini alikuwa tayari kuisaliti haki na kuwapendeza washitaki wake. Hii ilimweka katika upande mgungu. Na ule umati uling’amua sitasita yake. Kama mara ya kwanza Pilato angesimama imara na kukataa kumtia hatiani mtu asiye na hatia, angalikata minyororo wa majuto aliofungwa nao siku zote za maisha yake. Kristo angeuawa, lakini hatia isingalimkalia Pilato. Lakini Pilato alikuwa amechukua hatua baada ya hatua kudharau dhamiri yake, na sasa alijikuta asiyeweza cho chote mikononi mwa makuhani na wakuu.TVV 413.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents