Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shetani alikusudia kufaulu

    Tangu wakati ule Amiri jeshi wa mbinguni alipokuwa angali mtoto mchanga katika Bethlehemu, alikuwa katika mashambulio ya Shetani, Katika kikao cha Shetani iliazimiwa kuwa, lazima washinde. Majeshi ya malaika waovu walipangwa katika njia zote za Yesu ili kumpinga, na ikiwezekana kumshinda.TVV 57.2

    Katika ubatizo wa Yesu Shetani alisikia sauti ikishuhudia Uungu wa Yesu, kutoka kwa Yehova. Na sasa Yesu amekuja katika umbo la mwili wa dhambi, (Warumi 8:3). Baba mwenyewe alizungumza. Kwanza alisema na watu katika Kristo, sasa anasema nao katika hali ya kibinadamu ndani ya Kristo. Sasa ilidhihirika wazi kuwa mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu yamekamilika. Sasa Shetani aliona kuwa lazima ashinde au ashindwe. Juhudi zote za uasi zilitumika kumpinga Kristo.TVV 57.3

    Watu wengi waliangalia mashindano haya baina ya Kristo na Shetani kuwa ni jambo lisilowahusu. Lakini katika kila moyo wa mwanadamu, mashindano hayo yanahusika. Mitego na majaribu ambayo Yesu alishinda, ndiyo yanayotushinda leo. Yesu akiwa na nzigo wa dhambi za ulimwengu juu yake, alishinda jaribu la tamaa ya chakula, na la upendo wa dunia, na la kujionyesha ambako ni majivuno na kiburi. Majaribu hayo ndiyo yaliyomshinda Adamu na Hawa na ndiyo yanayotushinda sisi.TVV 57.4

    Shetani huonyesha kushindwa kwa Adamu kuwa ndio ushahidi wa kuthibitisha kwamba sheria ya Mungu haiwezekani kutiiwa. Katika hali ya kibinadamu Kristo alikukomboa kuanguka kwa Adamu. Lakini Adamu aliposhambuliwa na mjaribu, hakukuwa na laana ya dhambi kwake. Alikuwa mtu mkamilifu kabisa, mwenye mawazo kamili na mwili wa nguvu. Akizungukwa na utukufu wa Mungu, alikuwa akiwasiliana na viumbe wa mbinguni.TVV 57.5

    Haikuwa hivyo kwa Yesu alipokwenda jangwani kupambana na Shetani. Kwa muda wa miaka 4000 watu walikuwa wamedhoofishwa na dhambi kimwili na kiroho pia. Kwa hiyo walikuwa katika hali mbaya mno. Na Kristo alichukua maovu yao yote. Kwa njia hiyo aliweza kumwokoa mtu yeyote, hata yule aliyezama dhambini mno.TVV 57.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents