Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Viumbe vya asili vilifunua wito wa Biblia

    Mbele ya macho yake kulikuwa vitu vingi sana, ambavyo viliumbwa na Mungu. Yule aliyeviumba vitu vyote, alisoma maandiko yake mwenyewe aliyoandika katika nchi, bahari na angani. Alikusanya hazina ya sayansi kutoka katika mimea, wanyama, na watu. Mifano aliyopenda kutumia katika mafundisho yake ya kufafanua ukweli, yalionyesha kwamba aliunganisha mambo ya kiroho na viumbe vya asili na katika mazingira ya kila siku maishani.TVV 34.2

    Yesu alipokuwa akijaribu kufahamu sababu za mambo kadha wa kadha, ya mbinguni ndio yalikuwa msaidizi wake. Tangu mwanzoni kabisa alikuwa akizidi kukua kiroho, akiwa na neema na elimu ya kweli.TVV 34.3

    Kila mtoto anaweza kupata elimu, sawa na Yesu alivyopata. Tunapojaribu kuhusiana na Baba wa mbinguni, malaika watatusogelea, mawazo yetu yataimarishwa, na tabia zetu zitainuliwa na kutakaswa. Tutafanana naye zaidi na azaidi. Tunapotafakari uzuri, na ukubwa wa viumbe, mawazo yetu hupanda kwa Mungu. Roho zetu hupata kicho, nia zetu huimarishwa ili kumwendea Mungu, kwa njia ya kazi zake. Kushirikiana naye kwa njia ya sala, hukuza akili na nia kabisa.TVV 34.4

    Yesu alipokuwa mtoto alifikiri kama mtoto, na kunena kitoto, lakini hakuna na alama ya uovu katika hali yake, alikuwa na hali ya Mungu tu, ila hakutengwa mbali na majaribu. Wenyeji wa Nazareti walijulikana kwa ajili ya uovu wao. Soma Yohana 1:46. Ilimlazimu Yesu kujiangalia sana, ili ajikinge na maovu hayo. Alikabiliwa na mambo yote yanayotukabili sisi, bila kupotoka, ili awe kielelezo halisi kwetu, tangu utoto, hata ujana, na utu uzima.TVV 34.5

    Tangu utoto wake, Yesu alikuwa akilindwa na mbingu, kwa njia ya malaika, walakini maisha yake yalikuwa ya mashindano makali na uovu. Mkuu wa giza hakubakiza kitu chochote asichotumia kumpinga Yesu.TVV 34.6

    Yesu alifahamu hali ya umasikini, na kuzoeana nayo, pamoja na kujinyima. Hali hiyo ilimfaa sana na kumlinda. Hakujishughulisha na hali yoyote potovu. Yesu hakushughulika kutafuta starehe, mapato, wala heshima, au raha, maana vitu hivyo vingekuwa mtego wa kumtia dhambini. Ni Kristo peke yake aliyeishi katika mji mwovu wa Nazareti kwa miaka karibu thelathini, bila kutenda dhambi. Jambo hili ni kanusho kubwa kwa wenye udhuru wa kutenda dhambi wakisingizia mahali, kazi, mali au bahati.TVV 34.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents