Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Nafasi ya Mwisho Kuonyesha Huruma ya Kibinadamu

  Giza lilipomalizika, Kristo alisikia uchungu mwilini mwake, akasema, “Naona kiu.” Mmoja wa askari wa Kirumi akaona huruma, akachukua ufito wa hisopo uliokuwa na sifongo juu yake na akauchovya katika siki akampa. Lakini makuhani walidhihaki maumivu yake. Maneno aliyosema; “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” waliyatafsiri visivyo, wakasema: “Huyu anamwita Eliya.” Wakakataa nafasi ya mwisho ya kupooza maumivu yake. “Acha; na tuone kama Eliya anakuja kumwokoa.”TVV 428.1

  Mwana wa Mungu asiye na mawaa alitundikwa msala-bani, mwili wake ukiwa umepasukapasuka kwa kupigwa mijeledi; mikono ile ambayo mara kwa mara ilitumika katika kubariki, ikiwa imepigiliwa katika msalaba kwa misumari; ile miguu iliyotembea bila kuchoka katika huduma ya upendo, ikiwa imekongomewa mtini; ile midomo iliyotetemeka ilitoa kilio cha ole. Na yale yote aliyavumilia matone ya damu yaliyotiririka kutoka katika kichwa chake, mikono yake; miguu yake maumivu ya uchungu yalitikisa mwili wake, na uchungu usioelezeka ulioujaza moyo wake kwa sababu ya kufichika uso wa Baba yake humwambia kila mtoto wa Adamu, yakitangaza kwamba sababu yako Mwana wa Mungu alikubali kubeba mzigo huu wa hatia; kwa ajili yako aliangamiza mamlaka ya mauti; kwa ajili yako alifungua malango ya Paradiso; kwa ajili yako alijitoa mwenyewe kuwa kafara kutoka upendo kuja kwako.TVV 428.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents