Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    53 — Safari ya Mwisho Kutoka Galilaya

    Kadiri huduma yake ya duniani ilipokaribia kumalizika, Yesu alibadili kazi yake yaani aligeuza namna ya kufanya kazi. Pale na pale alikuwa akiepuka makutano ya watu wasimsifu, na aliwaagiza watu wasimtajetaje.TVV 275.1

    Wakati wa Sikukuu ya Vibanda alikuwa amefika Yerusalemu, bila kujidhihirisha yaani kwa siri. Lakini katika safari yake ya mwisho haikuwa kwa siri. Alisafiri waziwazi, akitangazika huko na huko, ambavyo haikuwa kawaida yake. Sasa alikuwa akienda mahali pa kujitolea kwake wakfu, na kwa hiyo lazima watu wafahamu sana.TVV 275.2

    “Kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye hana budi kuinuliwa. Yohana 3:14. Macho yote lazima yamwangalie, ili kuona kafara iliyotolewa kuleta wokovu katika ulimwengu uliopotea.TVV 275.3

    Wanafunzi wangalimkataza kwenda Yerusalemu. Walikuwa Wanajua uhasama mkubwa wa waongozi wa dini waliokuwa nao huko Yerusalemu. Kwa Yesu ilikuwa safari nzito sana kupeleka wanafunzi wake mahali pa namna hiyo, wakaone mambo ya kukatisha tamaa na huzuni vilivyomngojea Yesu huko Yerusalemu. Shetani alikuwa tayari kuhimiza majaribu hayo yampate Kristo. Kwa nini aende huko Yerusalemu kwenye hali kama hiyo? Kila upande kulikuwako na wenye dhiki wengi waliokuwa wakitaka kuponywa. Kwa nini asiende katika ulimwengu mpana, mahali anapoweza kunena neno lake na kuponya watu? Kwa nini asiende kuwaangazia watu mamilioni wanaokaa gizani? Adui za Kristo walimshambulia kwa ukali na majaribu ya hila. Kama Yesu angalibadili kusudi lake, na kufanya vinginevyo ulimwengu ungaliangamia kabisa.TVV 275.4

    Lakini Yesu amenuia kabisa kwenda Yerusalemu kwa vyovyote vile. Sheria yake imara ni kutenda mapenzi ya Baba yake peke yake. Tangu utoto wake, alimwambia Mariamu mama yake, “Hamjui ya kuwa inanipasa kuwa katika shughuli ya Baba yangu?” Luka 2:49. Lakini katika mpango mkuu wa Baba, kuhusu saa ya kujitoa kwa ajili ya kuwa kafara ya ulimwengu, ilikuwa karibu kufika.TVV 275.5

    Hamwezi kukosea, wala Baba pia hawezi. Adui zake wamepanga kumwua kwa muda mrefu, sasa muda umefika wa kutoa maisha yake.TVV 276.1

    Alituma wajumbe wamtangulie. Nao wakaenda, wakaingia mjini huko Samaria ili kumtayarishia. Lakini watu wa Samaria walikataa kumkaribisha, kwa sababu alikuwa akienda Yerusalemu; hawakufahamu kuwa walikuwa wakikikataa kipaji cha mbinguni. Lakini Wasamaria walipoteza yote kwa ajili ya chuki na ushindani wao.TVV 276.2

    Yakobo na Yohana waliokuwa wajumbe wa Kristo, waliudhika sana kwa jambo hilo. Walighadhabika kwa kuwa Yesu ametendwa vibaya kwa kukataliwa hivi, na Wasamaria. Walimwambia Kristo kuwa watu hao wamekataa hata kuwapa nafasi ya kulala usiku mmoja tu. Wakiuona mlima wa Karmeli ambako Eliya aliwateketeza manabii wa Baali ambao ni waongo, walisema: “Huwezi kuamuru moto utoke mbinguni na kuwateketeza wabaya hawa?” Halafu jibu la Yesu liliwashangaza aliposema, “Hamjui roho mliyo nayo, kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuangamiza watu, ila kuwaokoa.” Kisha akaenda katika kijiji kingine.TVV 276.3

    Siyo kazi ya Kristo kuwalazimisha watu wamwamini. Yeye hutaka watu wamwamini kwa hiari yao wenyewe kumfuata wakivutwa na upendo wao. Hakuna ushahidi mkubwa zaidi wa roho ya kishetani kuliko huu iwapo tunawachukia wale wasiokubaliana na sisi katika imani yetu, na kutupinga. Hakuna kitu kinachomchukiza Mungu zaidi kuliko wakristo kuwasumbua wale waliotiliwa na Kristo na kununuliwa kwa damu yake.TVV 276.4

    Miezi ya mwisho mwisho wa kufunga kazi ya Kristo, ilitumika zaidi katika sehemu ya Perea, wilaya ya ng’ambo ya Yordani kutoka Uyahudi. Tazama Marko 10:1. Hapo watu wengi walimfuata, na kazi yake ya kwanza ilirudiwa.TVV 276.5

    Kama alivyowatuma wale mitume kumi na wawili, ndivyo sasa alituma wengine sabini, akawaagiza wamtangulie, naye atafuata nyuma. Akawatuma waende wawili wawili katika kila mji. Watu hawa walikuwa katika mafundisho kuhusu kazi hiyo. Walikuwa na bahati ya kukaa pamoja naye na kusikiliza mafundisho yake.TVV 276.6

    Maagizo aliowaagiza wale kumi na wawili, yalikuwa kwamba, wapite kwa watu wa mataifa, au kwa Wasamaria. Lakini wale sabini hawakuagizwa hivyo. Ingawa Yesu alifukuzwa na Wasamaria, lakini upendo kwao hakupunguzwa. Aliwapenda kamili. Wale watu sabini kwa mara ya kwanza walikwenda katika miji ya Samaria wakalihubiri neno kwa jina lake.TVV 277.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents