Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dunia Tamasha; Mbingu Watazamaji

    Mbingu iliangalia Kafara akisalitiwa na kwa ukatili akikimbizwa kutoka mahakama moja hadi nyingine. Mbingu zilisikia dhihaka za watesi wake na kukanwa kwa kiapo na mmoja wa wanafunzi wake. Mbingu ilimwona Mwokozi akikokotwa huku na huko kutoka Ikulu mpaka jumba la hukumu, mara mbili kwa makuhani, mara mbili kwa Sanhedrini, mara mbili mbele ya Pilato na mara moja mbele ya Herode, akidhihakiwa, kupigwa, kuhukumiwa na kupelekwa kusulibiwa.TVV 431.2

    Mbingu iliangalia kwa mshangao Kristo, akiwa ametundikwa msalabani, damu ikitiririka kutoka katika jeraha za kichwani, mikononi na miguuni. Majeraha yake yaliachama kutokana na uzito wa mwili wake kuning’inia kwa mikono peke yake. Roho yake ilitweta chini ya uzito wa dhambi za ulimwengu. Mbingu yote ilijazwa na mshangao wakati Kristo alipoomba katikati ya mateso yake makali, kuwa “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo” (Luka 32:34).TVV 431.3

    Nguvu za giza zilizozunguka msalaba zilitupa kivuli cha kutokuamini mioyoni mwa watu. Wakala wa Shetani waliwafanya watu waamini kuwa Yesu ni mwenye dhambi mkuu hivyo amefanywa awe mtu wa kuchukiwa. Wale waliokuwa wakimdhihaki Kristo walijazwa na roho ya mwasi mkuu wa kwanza. Alichochea dhihaka zao. Lakini pamoja na hayo yote hakufaulu jambo lo lote.TVV 431.4

    Kama Kristo angaliruhusu jambo lo lote la Shetani ili kuepukana na mateso ya kutisha yaliyomsibu, adui angelishinda. Kristo aliinamisha kichwa chake na kukata roho, lakini alishikilia kikamilifu imani yake. “Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu mchana na usiku.” Ufunuo 12:10.TVV 431.5

    Shetani aliona kuwa hila zake zote zimefichuliwa. Alikuwa amejidhihirisha mwenyewe kuwa ni mwuaji. Kwa kuimwaga damu ya Mwana wa Mungu, alikuwa amejing’oa mwenyewe kutoka katika fadhili za wakaaji wambinguni. Tangu hapo hawezi tena kuwatokea njia ni malaika wakitoka mbele za Mungu na kuwashitaki ndugu za Yesu kuwa wamefunikwa kwa unajisi wa dhambi. Kiungo cha mwisho cha fadhili kati ya Shetani na wenyeji wa mbinguni kilikatwa.TVV 432.1

    Hata hivyo malaika hawakuelewa yale yote yaliyohusika katika hili pambano kuu. Kanuni zilizohatarishwa lazima zidhihirike waziwazi. Mwanadamu na pia malaika lazima waone wazi tofauti iliyoko kati ya Mkuu wa nuru na mkuu wa giza. Kila mtu hana budi kuchagua yule atakayemtumikia.TVV 432.2

    Mwanzoni mwa pambano kuu, Shetani alitangaza kwamba sheria ya Mungu haiwezekani kushikwa, na kwamba haki haipatani vema na rehema, na kwamba ikiwa sheria itavunjwa, itakuwa vigumu kwa mwenye dhambi kusamehewa. Ikiwa Mungu ataondoa adhabu ya dhambi, Shetani alisisitiza, hawezi kuwa Mungu wa haki. Shetani alisema kuwa watu wanapovunja sheria ya Mungu, ni uthibitisho kuwa sheria hiyo haiwezekani kushikwa; mwanadamu hawezi kusamehewa. Kwa sababu yeye, baada ya uasi wake, alifukuzwa kutoka mbinguni, Shetani alidai kuwa, binadamu sharti angetengwa milele na fadhili za Mungu. Mungu hawezi kamwe kuwa mwenye haki, na wakati ule ule aonyesha rehema kwa mwenye dhambi.TVV 432.3

    Lakini mwanadamu alikuwa katika hali tofauti na ile ya Shetani. Lusifa alifanya dhambi katika utukufu wa Mungu. Shetani aliamua kufuata mapenzi yake ya ubinafsi huku akiwa anaielewa tabia ya Mungu. Hakuna jambo lo lote zaidi ambalo Mungu angelifanya ili amwokoe. Lakini mwanadamu alidanganywa, mawazo yake yakiwa yamefumbwa kwa werevu wa Shetani. Hakuelewa urefu wala kina cha upendo wa Mungu. Kwa kuangalia tabia ya Mungu huenda ataweza kuvutwa amrudie Mungu.TVV 432.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents