Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wazazi wake wafadhaika

    Wakati ule walipotoka Yerusalemu kurudi nyumbani, Yusufu na Mariamu hawakuweza kumwona Yesu. Msukosuko wa safari uliwabana kiasi cha kutoshughulika kumwangalia mpaka kukachwa. Halafu hawakuona mtu wa kuwasaidia. Wao walidhani kuwa Yesu yumo katika msafara; kwa hiyo hawakuwa na wasiwasi. Lakini sasa mashaka yao yakaamka. Wakatetemeka, walipokumbuka jinsi Herode alivyojaribu kumwua wakati wa utoto wake. Wasiwasi ukawajaa tele.TVV 39.2

    Walianza kumtafuta, huku wakirudi kuelekea Yerusalemu. Siku ya pili, kukasikiwa sauti yake katika hekalu. Kumbe alikuwa katika shule ya walimu. Mama yake alisema kwa sauti ya kukemea: “Mtoto, kwani umetutendea hivi? Tazama baba yako na mimi tumekutafuta kwa huzuni sana.”TVV 39.3

    Yesu akajibu, “Kwani kunitafuta, hamjui kuwa inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” Walipoonekana kutofahamu maana yake, alielekeza kidole mbinguni. Uso wake uling’aa. Uungu uling’aa katika ubinadamu. Wamesikia maongezi yake na walimu wakuu, nao walishangaa kwa maswali yake na majibu.TVV 39.4

    Yesu alikuwa akishughulika na kazi aliyokuja kufanya; lakini Yusufu na Mariamu hawakujali kazi zao. Mungu amewaheshimu sana kwa kuwapa kazi ya kumtunza Yesu. Lakini walimpoteza mtoto kwa muda wa siku nzima, na hata walipomwona hawakufahamu kazi yake.TVV 39.5

    Lilikuwa jambo la kawaida kwa wazazi wa Yesu kumheshimu kuwa mtoto wao. Katika mambo mengi, hali ilikuwa hiyo kuwa kama mtoto wao tu, hivyo ilikuwa vigumu kumfahamu kuwa ni Mwana wa Mungu. Maneno ya upole aliyowaambia, yalikusudiwa kuwajulisha kuhusu kazi yake takatifu, na yao pia. jawabu la Yesu kwa mamaye, lilionyesha kuwa alifahamu uhusiano wake na Mungu. Mariamu hakufahamu maneno hayo yana maana gani; lakini alielewa kuwa Yesu ni mwana wa Yusufu, na kuwa anakubali kuwa ni Mwana wa Mungu.TVV 39.6

    Kutoka Yerusalemu, Yesu alirudi nyumbani na wazazi wake, akawa anawatii na kuwasaidia. Kwa muda wa miaka kumi na minane, Yesu alijulikana kuwa mwana wa Yusufu, mtoto wa Nazareti, akiwa mwenyeji na rafiki wa Nazareti.TVV 40.1

    Yesu alikusudia kurudi Yerusalemu katika hali ya ukimya pamoja na wale waliojua siri ya maisha yake. Kwa njia ya pasaka, Mungu alitaka kuwakumbusha watu wake kazi ya ajabu juu ya ukombozi wao kutoka Misri. Katika kazi hii alikusudia kuwaonyesha ahadi ya ukombozi kutoka dhambini. Damu ya Kristo ingewaokoa. Mungu alitamani wajifunze kazi ya Kristo kuhusiana na ukombozi wao kutoka dhambini. Lakini watu walipokwenda kutoka Yerusalemu mambo ya safari tu ndiyo yalikuwa katika nia zao, huduma waliyofanya ilisahauliwa. Hata Mwokozi hakufikiriwa.TVV 40.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents