Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi ya kutomjali Kristo

    Lakini Kristo huona yote hayo, naye huserna, Ni mimi niliyekuwa na njaa, na kiu. Ni mimi niliyekuwa, mgeni. Mlipokuwa mkijilisha kwa karamu za anasa, mimi, nilikuwa nikishinda na njaa kibandani. Mlipokuwa mkijifurahisha katika majumba yenu ya anasa, mimi sikuwa, na mahali pa kulala. Ninyi mlipokuwa mkishughulikia sikukuu, mimi nilikuwa nikisumbuka gerezani. Mlipotoa makombo ya chakula kwa masikini wenye njaa, na mavazi hafifu kwa watu waliopigwa na baridi, je mlitambua kuwa nilimfanyia hayo Bwana wa Utukufu? Katika maisha yenu yote, nilikuwepo miongoni mwa wenye dhiki, lakini hamkujali kunitafuta. Kwa hiyo hamwezi kuingia pamoja nami katika furaha. Siwajui ninyi.TVV 362.1

    Wengi hutembelea sehemu alizoishi Kristo hapa, duniani, wakiangalia ziwa ambako alikuwa akipenda kufundisha watu kando yake, na vilima na mabonde aliyoyaona. Lakini haitupasi kwenda Nazareti, au Bethania ili kutembea katika nyayo za Yesu. Tutazikuta nyayo zake kando ya kitanda cha mgonjwa, katika vibanda vya maskini, na po pote pale walipo wenye dhiki wanaohitaji faraja.TVV 362.2

    Wote,watapata jambo moja la kutenda. Watu mamilioni waishio katika kifungo cha ujinga na dhambi hawajapata kusikia habari za upendo wa Yesu kwao. Kanuni ya Kristo ya maisha ambayo kila mtu atahukumiwa nayo ni, “Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo.” Mathayo 7:12.TVV 362.3

    Mwokozi ametoa uhai wake ili kulisimamisha kanisa litakaloweza kuwahudumia wenye kujaribiwa. Waumini waweza kuwa maskini, wasiokuwa na elimu, na wasiojulikana, walakini katika Kristo wanaweza kufanya cho chote kwa majirani zao, na hata “katika nchi za mbali,” ambayo matokeo yake yatafika hata katika umilele. Kwa sababu kazi hii imedharauliwa, waamini wapya hawajishughulishi hata kidogo katika kupiga hatua ya uzoefu wa maisha ya Kik:risto. Juhudi mpya ambayo kila mara huleta hatari inaweza kuelekezwa kuwa vijito vya mibaraka. Ubinafsi ungesahauliwa, katika juhudi za kuwahudumia wengine. Wale wanaowahudumia wengine wasingekuwa na haja ya kutamani michezo ya msisimko au kuwa na mabadiliko maishani mwao. Kusudi lao kuu lingekuwa namna ya kuwaokoa watu kutoka katika hatari ya upotevu.TVV 362.4

    Mfalme wa utukufu alikuja kuishi na sisi, ili kutufanya kuwa jamaa moja. Naye alisema: “Mpendane kama nilivyowapenda ninyi.” Yohana 15:12. Kama tukiupenda ulimwengu kwa jinsi ile Yesu alivyotupenda, tutatimiza kazi yake. Tutafaa kwenda mbinguni, maana tunayo mbingu katika mioyo yetu. Katika siku ile kuu ya hukumu, wale ambao hawakumfanysia kazi Kristo walioishi kwa ubinafsi kwa kujifikiria wenyewe, watawekwa na Hakimu wa ulimwengu wote katika upande wa watenda maovu.TVV 363.1

    Kwa kila mtu umekabidhiwa wajibu. Kwa kila mtu Mchungaji mkuu atauliza. “Liko wapi kundi lako ulilopewa, kundi lile zuri?” Yeremia 13:20.TVV 363.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents