Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mtu mfu amefufuliwa

  Zaidi ya maili ishirini kutoka Kapernaumu palikuwako na mji wa Naimi, hapo Yesu alipumzika. watu walikuja kutoka katika njia yote, wakileta wagonjwa wao ili waponywe, na hapo wakitumaini kuwa Yesu atajidhihirisha kuwa ndiye Mfalme wa Israeli. Kundi lenye furaha lilimfuata katika njia yote ipitayo miambani mpaka kwenye mji wa mlimani.TVV 171.7

  Walipokaribia waliona jeneza linachukua maiti kwenda makaburini. Katika jeneza mlikuwamo maiti. Watu walikuwa wakilia sana, kuonyesha masikitiko yao kwa mtu aliyekufa.TVV 172.1

  Maiti alikuwa mwana pekee wa mama yake, na mama huyo alikuwa mjane. Mama aliyefiwa alikuwa akifuatana na maiti mpaka makaburini. “Bwana alipomwona alimhurumia.” Alipoendelea alimsogelea, akamwambia, “Usilie.”TVV 172.2

  “Akaenda, akalishika jeneza.” Kwa Yesu kugusa mtu mfu hakutamtia unajisi wowote. Waliolichukua jeneza wakasimama na kundi lote lililokuwa likilia likakusanyika likitumaini jambo fulani. Aliyekuwa akifukuza pepo alikuwako, je hata kifo pia kinashindwa na uwezo wake?TVV 172.3

  Alitamka maneno kwa sauti ya mamlaka, akisema: “Kijana, nakuagiza, Ondoka.” Sauti hiyo ilipenya masikioni mwa mfu. Kijana akafungua macho. Yesu akamshika mkono, akamwinua, mama yake akamkumbatia kwa furaha. Makutano wakaangalia kwa mshangao, kana kwamba wako mbele za Mungu. Kisha wakamhimidi Mungu, wakisema: “Nabii Mkuu ametujia, na Mungu amewajia watu wake.” Waliokuwa wakichukua jeneza wakarudi Naini kwa furaha kuu.TVV 172.4

  Aliyekuwa akisimama kwa mama aliyekuwa akilia huko Naini, huguswa na masikitiko yetu leo. Maneno yake leo yanafaa sana kama yalivyofaa kwa kijana wa Naini. Tazama Mathayo 28:18. Kwa watu wote wanaomwamini yeye ni Mwokozi yule yule aliye hai.TVV 172.5

  Kijana yule alirudishwa kuwa mzima katika nchi hii, akishindana na matatizo ya dunia na kupitia katika nguvu za mauti. Lakini Yesu hutufariji katika matatizo na huzuni za mauti kwa maneno haya: “Mimi ndimi aliyekuwa amekufa, nami sasa ni hai. tazama Mimi ni hai milele hata milele nami.. ninazo funguo za kuzimu na za mauti. Ufunuo 1:18.TVV 172.6

  Shetani hawezi kumshikilia mtu katika mauti ya kiroho, yule anayemshikilia Kristo kwa imani, na maneno yake yenye uwezo yakiwa moyoni mwake. “Amka wewe usinziaye, ufufuke katika wafu ...” Waefeso 5:14. Maneno ya Kristo yaliyomwamuru mtu wa kwanza akawa hai, yangali yanatoa uzima. Maneno ya Kristo kwa kijana yule, kwamba: “Kijana nakuagiza ondoka”, yakampa kijana wa Naini uzima, ndivyo ilivyo kwa maneno kwamba Inuka kutoka katika ufu, hutoa uzima kwa mtu anayeyapokea.TVV 172.7

  Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka ufuni akikaa ndani yenu, yule aliyemfufua Kristo kutoka ufuni ataifufua miili yenu. Soma Warumi 8:11; 1 Wathesalonike 4:16, 17. Hayo ndiyo maneno yenye kutufariji sisi kwaTVV 173.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents