Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    85 — Kando Ya Bahari Tena

    Yesu alikuwa amepanga kukutana na wanafunzi wake huko Galilaya. Kutokuwako Yerusalemu wakati wa Juma la Pasaka kungesababisha wanafunzi kueleweka kuwa ni waasi wakana imani. Lakini baada ya kumalizika shughuli za Pasaka wanafunzi walifurahi kurudi nyumbani kukutana na Mwokozi kama alivyoagiza. Wanafunzi saba walifuatana. Walikuwa maskini kulingana na utajiri wa dunia hii lakini matajiri katika maarifa ya ukweli. Kwa muda wa miaka mitatu walikuwa wamefundishwa na Mwalimu Mkuu ambaye ulimwengu ulikuwa haujapata kumwona. Walikuwa wenye uwezo na makini, wakala ambao kwao wanadamu wataongozwa kupata maarifa ya kweli.TVV 457.1

    Wanafunzi walikusanyika mahali patulivu ambapo pasingekuwa na ghasia yo yote. Mbele yao ilikuwa ni pwani ambapo watu zaidi ya elfu kumi walilishwa kwa mikate michache na samaki. Siyo mbali sana na ulipokuwa mji wa Kapernaumu, kulikofanywa miujiza mingi.TVV 457.2

    Petro ambaye bado alikuwa anapenda sana mashua na hamu ya kuvua alipendekeza kuwa waende baharini wakavue kidogo. Walihitaji chakula na mavazi, ambavyo vingepatikana kutokana na mauzo ya kazi hiyo. Hivyo walienda; lakini usiku kucha walisumbuka bila kuambulia cho chote. Katika saa ya taabu zao waliongea juu ya kutokuwepo kwa Bwana wao. Walizungumzia hali yao ya siku za mbele, wakawa na wasiwasi jinsi mambo yalivyokuwa yakiwaendea.TVV 457.3

    Hatimaye kukapambazuka Mashua ikakaribia pwani, wanafunzi wakaona mgeni amesimama pwani, ambaye aliwasemesha kwa kuwauliza “Wanangu mna kitoweo?” Walipojibu kuwa La, “akawaambia, “Litupeni jarife upande wa kuume wa chombo, nanyi mtapata.” Basi, Wakatupa; wala sasa hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki. Yohana akamtambua mtu yule na akamwambia Petro, “Ndiye Bwana.” Petro alifurahi kiasi kwamba akajitupa majini na kuogelea, kitambo alimfikia Bwana. Wanafunzi wengine walikuja wakilikokota jarife lao lililojaa samaki. Wakaona huko moto wa makaa na juu yake pametiwa samaki na mkate.TVV 457.4

    “Yesu akawaambia, Leteni hapa baadhi ya samaki mliowavua sasa hivi.” Petro akakimbilia jarife na kuvuta mpaka pwani. Baada ya hayo Yesu akamega mkate na kuwagawia wote, na wote saba wakamtambua. Lakini walishikwa na mshangao sana, na kwa kimyakimya wakamtazama Mwokozi aliyefufuka.TVV 458.1

    Wakakumbuka vizuri wakati ule Yesu alipowaita kando ya bahari na kuwaambia, “Wamfuate.” Alikuwa amewaita waziache nyavu na mashua zao, na alikuwa ameahidi akawafanya wavuvi wa watu. Ili kuwakumbusha kisa hiki na kukazia wito wao, alirudia tena kufanya muujiza ili kufanya upya wito wake kwao. Kifo cha Bwana wao hakika hakikuondoa wajibu wa kufanya kazi aliyowapa. Ijapokuwa walikosa kazi ya kupatia mahitaji yao ya kila siku, kutokana na kuacha kazi yao ya awali, Mwokozi aliyefufuka atawapatia mahitaji yao yote. Ikiwa watatenda kazi pamoja naye, hawatashindwa kufaulu.TVV 458.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents