Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  87 — Kristo Aingia Mbinguni Kwa Ushindi

  Muda ulikuwa umefika kwa Kristo kupaa, kwenda kwa kiti cha enzi cha Baba yake kama Mungu mshindi. Baada ya kufufuka kwake alikaa duniani kwa muda ili wanafunzi wake wamzoee akiwa na mwili wa utukufu. Sasa alifikia wakati wa kuondoka. Wanafunzi wake hawakupaswa tena kuendelea kumhusisha na kaburi. Waanze kumfikiria kama aliyetukuka mbele za mbingu. Kama mahali pa kupalia kwenda mbinguni Yesu alichagua pale alipokuwa akizoea kwenda alipoishi duniani, yaani Mlima wa Mizeituni. Vichaka na vibonde vyake vilikuwa vimewekwa wakfu kwa maombi na majozi yake. Katika bustani ya Gethsemani, chini ya mlima huu alikuwa ameomba kwa uchungu mkuu peke yake. Juu ya kilele chake ndipo miguu yake itakapokanyaga arudipo mara ya pili, akiwa Mfalme wa utukufu wakati haleluya za Waebrania zitakapounganika na Hosana za wamataifa na jeshi kubwa litakapoitikia kwa sauti, Mvikeni taji Bwana wa wote!TVV 468.1

  Sasa Yesu na wanafunzi wake walianza safari kuelekea mlimani. Walipokuwa wakipita katika malango ya Yerusalemu watu wengi walikuwa wakiwaangalia kwa mshangao wakiongozwa na yule ambaye majuma machache kabla ya hapo wakuu walikuwa wamemsulibisha. Wanafunzi hawakujua kuwa hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuzungumza na Bwana wao. Yesu alitumia muda akikaa pamoia nao, akiyarudiarudia mafundisho yake. Walipokaribia Gethsemane, Alisimama. Aliuangalia mzabibu aliokuwa ameufananisha na mwungano wa kanisa lake na yeye na Baba yake. Tena akarudia ukweli aliokuwa ameufunua.TVV 468.2

  Kristo akiishi ulimwenguni kwa miaka thelathini na mitatu alikabiliana na fedheha, matusi na dhihaka. Alikuwa amekataliwa na kusulibishwa. Sasa alikumbuka hali ya utovu wa shukrani ya watu aliokuja kuwaokoa, je atawaondolea huruma yake na upendo wake? La; ahadi yake ni kwamba “Mimi nipo pamoja nanyi siku zole hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28:20.TVV 468.3

  Walipofika Mlima wa Mizeituni, Yesu aliwaongoza mpaka kileleni kukabili jirani na Bethania. Hapa alisimama na wanafunzi wakamzunguka. Aliwatazama kwa upendo. Hakuwalaumu kwa makosa yao au kushindwa kwao; maneno ya huruma kuu, rehema aliyowambia yalikuwa ndiyo ya mwisho kudondoka kutoka kinywani mwa Bwana wao. Akiinyosha mikono yake juu yao katika kuwabariki, na kana kwamba anawahakikishia ulinzi wake kwao, Aliinuliwa taratibu kutoka kwao, akivuta kwenda mbingu kwa nguvu kuu kuliko uvutano wo wote wa duniani. Alipokuwa akipanda wanafunzi walimkodolea macho mara ya mwisho Bwana wao. Wingu la utukufu likamficha na alipokuwa akipokelewa na gari la wingu tukufu la malaika maneno yafuatayo yakasikika “Tazamia mimi nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahari.” Wakati huo huo wimbo mtamu kuliko zote ukawamwagikia kama burudiko tulivu kutoka kwa kwaya ya malaika.TVV 469.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents