Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    36 — Mguso wa Imani

    Yesu aliporudi upande wa Magharibi wa ziwa kutoka Gergesa, aliwakuta makutano yamekusanyika wakimngojea. Alikaa pwani muda kitambo, akiwafundisha watu na kuponya maradhi yao. Kisha akaenda nyumbani kwa Lawi Mathayo ili kuhudhuria katika karamu. Hapo Yairo mkuu wa sinagogi alikutana na Yesu. Akiwa na masikitiko makubwa, alimwambia, “Binti yangu yumo katika hali ya kufa. Nakuomba uje uweke mkono wako juu yake ili apone; naye aishi.”TVV 189.1

    Yesu akaondoka mara moja kwenda kwa Yairo. Wanafunzi wake walistaajabu kwa ukubali wake wa kwenda kwa Rabi huyu, walakini walifuatana na Mwalimu wao, na kundi la watu pia. Yesu na wanafunzi wake waliendelea pole pole sana, maana makutano walikuwa wakimsonga pande zote. Baba wa mgonjwa alikuwa na wasiwasi kwa kusimama mara kwa mara kwa Yesu ili kuwasaidia wenye dhiki, au kuwafariji wenye mashaka.TVV 189.2

    Wakati walipokuwa wangali njiani, mjumbe alifika na kutoa habari kuwa binti wa Yairo amekwisha kufariki. Yesu alisikia hivyo, akasema: “Usiogope, amini tu, binti yako atapona.”TVV 189.3

    Basi wakaenda kwa haraka mpaka nyumbani kwa mkuu huyo. Waombolezaji walikuwako tayari wamgjaza mji na makelel. Yesu alijaribu kuwayama-zisha, akisema: “Mbona mnafanya ghasia hiVi? Msichana hakufa, ila amelala.” Walichukizwa kwa maneno ya mgeni huyu. Wamemwona kijana akifa wazi. Yesu alipotaka waondoke wote, aliwachukua babaye na mamaye, pamoja na Petro, Yakobo na Yohana, wakaingia pamoja katika chumba alimolala marehemu.TVV 189.4

    Yesu alikaribia kitanda cha maiti, akaukumbatia mkono wake kama deaturi yao, akasema: “Msichana, nakauagiza ondoka.”TVV 189.5

    Akaondoka mara moja kwa kutetemeka, akapita katika watu wenye kushangaa, macho yake yamekodolewa sawa na mtu atokaye usingizini, akiangaliwa kwa mshangao mkubwa na watu wote waliokuwa hapo. Wazazi wake wakamkumbatia kwa furaha isiyosemeka.TVV 190.1

    Walipokuwa njiani wakienda kwa mkuu huyu, Yesu alikutana na mwanamke maskini, ambaye alikuwa amesumbuliwa na ugonjwa kwa muda wa miaka kumi na miwili. Alikuwa ametumia mali yake yote kwa waganga bila kupona. Lakini aliposikia kuwa kristo yuko, akawa na matumaini. Kama angemfikia tu angepona. Kwa shida akajikokota pole polae mpaka pwana. Yesu alipokuwa akifundisha watu, akajaribu kumsogelea, asiweze. Akamfuata katika nyumba ya Lawi Mathayo, lakini hata huko hakuweza kumfikia kwa asababu ya makutano. Alikuwa katika kukata tamaa, wakati Yesu aliposogea karibu naye.TVV 190.2

    Alikuwa karibu na Mganga Mkuu! Lakini kwa ajili ya ghasia nyingi na fujo kubwa, hakuweza kusema naye, wala kutazamana naye. Akiwa na hofu na wasiwasi wa kutokubaliana naye na kumweleza hali ya matatizo yake, alijisogeza kuelekea kwake, huku akijisemea mwenyewa: “Nikimgusa pindo la vazi lake, nitapona.” Yesu alipokuwa akipita, mwanamke huyu alinyosha mkono wake, akaweza kugusa upindo wa vazi lake. Katika mguso huo, ndipo alipoweka tumaini lake lote. Wakati huo huo udhaifu wake na ugonjwa wake ukapona kabisa.TVV 190.3

    Akajaribu kuondoka katika mkutano huo kwa furaha ya moyo wake, lakini wakati huo huo Yesu alisimama. Akiangalia huku na huku, aliuliza kwa sauti ya kusikika: “Nani amenigusa?” Swali hilo lilionekana kuwa ni swali la kigeni, maana alikuwa akisongwa-songwa na makutano pande zote.TVV 190.4

    Petro aliyekuwa tayari kusema, alisema: “Bwana makutano yanakusonga-songa, nawe wauliza: “Nani amenigusa?” Yesu alisema, “Maana naona nguvu zimenitoka”. Mwokozi aliweza kutambua mguso wa imani, na miguso-guso tu ya kawaida. Mguso wa imani hauwezi kupita ovyo tu. Angesema mwanamke huyu maneno ya faraja yataka yodumu mpaka mwisho wa dunia.TVV 190.5

    Akiwaangalia watu, Yesu aliweza kutambua yule aliyemgusa. Alipoona kuwa amefahamiwa, mwanamke alijitokeza wazi, akaja akitetemeka, akaeleza habari za ugonjwa wake, na jinsi alivyopata waokovu kwa Yesu. Ndipo Yesu akasema. “Binti.... Imani yako imekupnya, nenda zako kwa amani.” Hakumpa nafasi ya kueleza kwamba kuponywa kwake kumetokana na mambo ya ushirikina ya kugusa nguo na kupata uwezo wa kupona kimwujiza. Imani kamili ya kutegemea uwezo wa Mungu ndiyo imemponya.TVV 190.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents