Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    23 — Jinsi Danieli Alivyomtambua Yesu kuwa ni Kristo

    Kuja kwa Masihi kulitangazwa mara ya kwanza katika Yuda. Juu ya milima ya Bethlehemu malaika walitangaza kuzaliwa kwa Yesu. Katika Yerusalemu mamajusi walikuja kumtafuta.TVV 123.1

    Kama waongozi wa Israeli wangelimpokea Kristo, angaliwatuma kama wajumbe wake kuitangaza Injili duniani pote. Lakini hawakufahamu majira ya kujiliwa kwao. Wivu na kutoamini kwa viongozi wa Israeli vilitokeza chuki, na roho za watu ziligeukia mbali kutoka kwa Yesu. Baraza la Sanhedrin liliidhinisha kuuawa kwake. Kwa hiyo Yesu aliondoka kutoka Yerusalemu; kwa watu waliofundishwa sheria ya Mungu, akaligeukia taifa jingine kutangaza ujumbe wake.TVV 123.2

    Kwa kila kizazi, historia ya Kristo kujitenga na Yuda zilitangazwa. Wakati watengenezaji wa dini walipohubiri neno la Mungu, hawakuwa na wazo la kujitenga na kanisa, lakini viongozi wa kanisa hawakukubaliana na nuru hiyo mpya, na hao waliokuwa na nuru hiyo, walipaswa kutafuta watu wanaokubaliana na ukweli huo. Siku zetu hizi ni watu wachache tu baina ya wafuasi watengenezaji wa kanisa, yaani Reformers, husikia sauti ya Mungu, na kuwa tayari kukubaliana na neno linalohubiriwa. Kila mara wale wanaofuata hatua za watengenezaji hulazimishwa kutengana na makanisa yao, ili waweze kuhubiri neno la Mungu. Wengi hutoka na kutengana na makanisa ya baba zao, ili wapate kumtii Mungu.TVV 123.3

    Watu wa Galilaya walikuwa waelekevu sana kwa kazi ya Mwokozi. Waliokuwa na uhuru kutokana na wazazi wao, walilipokea neno la Mungu kamili. Huko Galilaya kulikuwa na mchanganyiko wa watu zaidi kuliko ilivyokuwa Uyahudi.TVV 123.4

    Yesu alipozunguka zunguka Galilaya, akifundisha na kuponya watu wengi walimfuata hata kutoka Uyahudi pia. Watu walisisimka kwa nguvu sana, hata ikabidi kujihadhari wasije wakaamsha wasiwasi kwa Warumi, wakidhani kuwa kutatokea mapinduzi. Wenye njaa na kiu ya haki, walilishwa neema ya Mwokozi mwenye huruma.TVV 123.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents