Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    5 — Yusufu na Mariamu Wamweka Wakfu Yesu

    Wakati Yesu alipotimiza siku arobaini baada ya kuzaliwa kwake, Mariamu na Yusufu walikwenda Yerusalemu ili kumkabidhi kwa Bwana, na kutoa sadaka. Jinsi Kristo alivyokuwa badala ya binadamu lazima aambatane na sheria katika mambo yote. Alikuwa ametahiriwa tayari, kuambatana na sheria.TVV 24.1

    Kama sadaka ya mama, kulitakiwa kutolewa kondoo wa kuteketezwa, au hua kwa ajili ya sadaka. Sadaka hizi zingekuwa hazina kasoro, maana zinamwakilisha Kristo. Yeye alikuwa ‘Mwana kondoo asiyekuwa na mawaa.” 1 Petro 1:19. Alikuwa kielelezo cha jinsi Mungu alivyokusudia ubinadamu kuwa kufuatana na utii kwa sheria yake.TVV 24.2

    Kuweka wakfu mzaliwa’ wa kwanza, kulianza zamani sana. Mungu aliahidi kumtoa mzaliwa wa kwanza ili kuokoa ulimwengu, wenye dhambi. Tendo hili ilipaswa kuheshimiwa na kila mtu kwa ajili ya kumtoa mzaliwa wa kwanza. Naye angekuwa kuhani; kama mfano wa Kristo kati ya watu.TVV 24.3

    Jambo hili lilielekea kwa Kristo wima namna gani! Lakini makuhani hawakuona maana yake, ni kama wamezuiwa na pazia. Kila siku kuhani alifanya mfano huu bila kujali wazazi, labda wawe ni matajiri au wakuu. Yusufu na Mariamu walikuwa maskini, na kuhani aliwaona kama watu wa Galilaya tu, wamevaa mavazi ya kawaida.TVV 24.4

    Kuhani alimshika mtoto mikononi mwake na kumwinua madhabahuni. Baada ya kumrudisha kwa mama yake, aliandika jina, “Yesu” katika orodha yake. Hakufikiri kuwa mtoto anayemwandika liikuwa Mtukufu wa mbinguni, aliye asili ya ukuu wa Wayahudi.TVV 24.5

    Mtoto huyu ndiye aliyesema kwa Musa, “Mimi Ndiye.” Aliyewaongoza Waisraeli kama wingu na kama nguzo ya moto. Ndiye alikuwa Tunu ya watu wote, shina la Daudi, mwenye kung’aa, Nyota ya asubuhi. Mtoto mchanga huyu ndiye alikuwa tumaini la wanadamu walioanguka. Atalipa kafara ili kuuokoa ulimwengu wote.TVV 24.6

    Lakini ingawa kuhani hakuona kitu chochote kwake kilichomvutia, wakati huo hakupita bila kumtambua Kristo. Kulikuwa na mtu katika Yerusalemu jina lake Simeoni . . . Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. Naye alifunuliwa na Roho Mtakatifu kwamba, hatakufa, kabla hajamwona Kristo.TVV 25.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents