Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kwa nini mtini huo ulilaaniwa

  Mitini isiyokuwa na majani haikuamsha tegemeo wala kukatisha tamaa. Hii ilisimama badala ya wamataifa, waliokuwa fukara wa utauwa kama vile Wayahudi. Pamoja nao “wakati wa tiini” ulikuwa bado. Walikuwa bado wanasubiri nuru na tumaini. Wayahudi, waliokuwa wamepokea mibaraka mingi zaidi kutoka kwa Mungu, walipaswa kuwiwa kwa kukufuru karama hizi. Nafasi waliyojivunia iliongeza tu hatia yao.TVV 326.7

  Yesu alikuja kwa Waisraeli akitumaini kuona kwao matunda yapasayo toba. Kila aina ya baraka walipewa, naye alitumaini kuona kwao hali ya kujinyima, rehema na kuwashughulikia watu wenzao ili wapate wokovu. Lakini upendo wa Mungu na upendo wa watu wenzao ulikuwa umefunikwa na kiburi na ubinafsi. Ukweli wa thamani waliopewa hawakuutoa kwa watu wengine wa ulimwengu. Kwa mfano wa mtini usiozaa wangaliweza kutambua makosa yao na adhabu watakayopata. Mtini uliolaaniwa ulikauka mpaka shina lake. Mfano huo ulionyesha jinsi Waisraeli watakavyokuwa wakati neema ya Mungu itakapoondolewa kwao. Kutoshirikisha mibaraka yao kwa wengine wasinga-liweza kupata mingine. Bwana asema: “Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, ya kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako,” Hosea 13:9.TVV 327.1

  Tendo la Kristo la kuulaani mtini aliouumba yeye mwenyewe, husimama kama onyo kubwa kwa makanisa na kwa Wakristo wote. Kuna watu wengi ambao hawaishi maisha ya Kikristo yasiyo na unafiki wala ubinafsi. Wakati ni wa manufaa kwao tu, wanapoweza kujipatia faida. Katika mambo yote ya maisha yao, hili liwe ndilo kusudi lao. Mungu anakusudia kwamba wawasaidie wanadamu wenzao kwa hali zote iwezekanavyo. Lakini ubinafsi huwafanya wasione kitu hicho, ila kujitumikia wenyewe peke yao. Wale wanaoishi kwa njia hiyo ya ubinafsi hufanana na mtini ule. Huonekana kuwa na mfano wa dini, isiyokuwa na imani, wala toba ya kweli. Hukiri kwamba wanamjua Mungu, lakini wakikana nguvu zake. Maneno Kristo aliyotamka kwa mtini, alisema kuwa mtu anayetenda dhambi kiwazi ana heri kuliko mtu anayedai kuwa anamtumikia Mungu bila kuzaa matunda ya haki, yanayoonyesha utukufu wake.TVV 327.2

  Mfano wa mtini usiozaa uliosemwa na Yesu kabla ya kwenda Yerusalemu, unaofuatana na fundisho la kuulaani mti usiokuwa na matunda. Kwa ajili ya mti usiozaa, mkulima alisema: “Hebu, uuache mwaka huu nao niupalilie, na kuutilia samadi. Ukizaa matunda mwaka ujao vema, la usipozaa ndipo utaukata.” Luka 13:8, 9. Mti huo utashughulikiwa. Katika mfano shughuli ya mtunza bustani haikuelezwa, ilitegemea watu ambao Kristo alisemea maneno hayo, ambao walifananishwa na mti usiozaa. Ilitegemea juu yao kuchagua mambo yao. Kila shughuli ilitolewa kwao lakini haikufaa kitu kwao. Katika tendo la Kristo la kuulaani mtini usiokuwa na matunda, matokeo yake yalionekana. Wao waliamua juu ya mambo yao ya baadaye, yaani kuangamia.TVV 327.3

  Kwa muda wa zaidi ya miaka elfu moja Wayahudi walikuwa wamekataa maonyo ya Mungu, na kuwaua manabii wake. Kwa dhambi zile zile, watu wa siku za Kristo walijionyesha kufuata njia ile ile. Mali ile watu wa Israeli waliyokuwa nayo kwa miaka mingi sana, ndiyo na watu wa siku za Kristo walikuwa nayo.TVV 328.1

  Kunakuja wakati ambao rehema ya Mungu hukoma kuita. Ndipo sauti pole ya Roho Mtakatifu ya kuwasihi wenye dhambi watubu hukoma. Siku kama hiyo ilikuwa imekuja kwa wenyeji wa Yerusalemu. Yesu aliwalilia kwa huzuni kuu watu ambao wanakabiliwa na maangamizo. Lakini haikufaa kitu. Katika kukataa maonyo ya Mungu, Israeli ilikataa njia ya kuwasaidia.TVV 328.2

  Taifa la Wayahudi lilikuwa mfano wa watu wa karne zote wanaodhihaki wito wa Upendo Mkuu. Machozi ya Kristo alipoulilia Yerusalemu yalikuwa ni kwa ajili ya dhambi za nyakati zote.TVV 328.3

  Katika kizazi hiki watu wengi husafiri katika barabara ile Wayahudi waliyosafiri bila kujali. Roho Mtakatifu amewazungumzia, bila kujali. Wamekataa maonyo na wajumbe wa Mungu. Leo ukweli wa Biblia, dini ya Kristo, hushindana na mkondo mzito wa ufedhuli. Hali mbaya ya kuchukia neno la kweli, sasa inazidi kuliko wakati wa Kristo. Neno la Mungu linalopingana na mawazo yao linakataliwa wazi, na watu huchagua wapendavyo lakini kwa uangamivu wao.TVV 328.4

  Wale waliopinga neno la Kristo walipata sababu nyingi kuhusu upinzani wao, mpaka wakatengana na Kweli na Uzima. Mungu hakusudii kuondoa kila kitu watu wanachotoa kama udhuru. Wale wanaokataa nuru ya neno la Mungu watabaki gizani milele. Kwao neno la kweli limefichika.TVV 328.5

  Maneno ya Kristo humhusu kila mtu anayedharau mwito wa Mungu wa rehema. Kristo anatoa machozi kwa ajili yako, wewe usiyejililia mwenyewe. Kila aina ya uthibitisho wa Mungu, na kila mwali wa nuru ya Mungu hukung’arisha au hufifia na kukuacha katika giza la milele.TVV 328.6

  Kristo aliona kuwa Yerusalemu utadumu kuwa mkaidi hivyo, lakini maovu yote yanaukalia mlangoni. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa watu wote wanaofuata njia ya namna hiyo. Bwana anasema: “Ee Yerusalemu mwenye kuwaua Manabii umejiharibu mwenyewe.” “Sikia ee nchi, tazama nitaleta maovu juu ya watu hawa, kuwapa matunda ya roho zao, kwa sababu hawakunisikia, wala maneno yangu, wala sheria yangu; lakini wameikataa.” Hosea 13:9; Yeremia 6:19.TVV 328.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents