Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mahakama yashindwa kumtisha Yesu

    Wayahudi walidhani kuwa, hali yao ya kuwa na dini ya nje tu wanao uzima wa milele. Lakini kwa kuwa wamemkataa Kristo katika neno lake, wamemkataa Yeye hasa. Alisema: “Hamji kwangu ili mpate uzima.”TVV 114.1

    Viongozi wa Wayahudi walijifunza unabii, si kwa kutaka kufahamu, ila kwa kutafuta mambo yenye kuwasaidia katika mipango yao. Kristo alipokuja kwa njia tofauti na matazamio yao hawakumpokea, ila walijaribu kuona kuwa ni mwongo. Kadiri Mwokozi alivyowasuta katika kawaida zao, ndivyo walivyozidi kuikataa nuru.TVV 114.2

    Yesu alisema: “Siupokei utukufu wa wanadamu.” Yeye hakutafuta ukubali wa Sanhedrin. Yeye alivikwa na utukufu wa mbinguni. Kama angeliutamani utukufu huo, malaika wangalimpa. Lakini kwa ajili ya faida yao alitaka Wayahudi wafahamu tabia yake.TVV 114.3

    Alisema: “Nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamkunipokea.” Wengine wakija wakitaja kuwa na tabia yangu, ila wakitafuta mambo yao, hao huwapokea. Kwa nini? Kwa sababu watafutao mambo yao hukubaliana na ninyi. Wayahudi huwakubali walimu wa uongo, kwa sababu huwasifu. Kwa kuwa mafundisho ya Kristo ni ya kiroho, hutaka kajinyima nafsi, kwa hiyo hayakubaliwi. Kwao sauti yake ni sauti ngeni.TVV 114.4

    Je, siku hizi hawako walimu wa dini wanaolikataa, neno la Mungu, na kufuata mapokeo yao?TVV 114.5

    “Kama mngalimwamini Musa mnganiamini na mimi, maana aliandika mambo yanayonihusu. Lakini kwa kuwa hamwamini maneno yake, mtayaaminije maneno yangu?” Kama wangeliyaamini maneno ya Mungu yaliyosemwa kwa njia ya kiongozi wao mkuu, wangefahamu mafundisho ya Kristo. Makuhani na marabi waliona kuwa upinzani wao kwa Kristo hauna maana, walakini chuki yao ya uuaji ilizidi tu kuwachochea. Waliogopa walipoona kuwa kuna uwezo mkuu katika kazi yake, lakini walizidi kujifungia gizani.TVV 114.6

    Walikuwa wameshindwa kuupindua uwezo wa Yesu, wala kuzuia watu wasimfuate. Wengi walikuwa wameongolewa kwa maneno yake. Wakuu hao walishindwa kabisa kumhukumu Kristo, walakini walikusudia tu kumwulia mbali. Walituma watu ili wawahadhari watu juu ya Yesu, kuwa mtu mlaghai tu, siye mtu wa kweli. Walituma wapelelezi kuona anachofanya na mambo anayosema. Mwokozi wa thamani, alikuwa sasa katika uvuli wa mauti ya msalaba.TVV 114.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents