Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Bila Kutambulika, Yesu Afafanua Maandiko

  “Kisha akawaambia, Enyi msiofahamu wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya, na kuingia katika utukufu wake?” Huyu anaweza kuwa nani mwenye kueleza mambo haya kinaganaga hivi na kwa huruma? Kwa mara ya kwanza wakaanza kuwa na tumaini. Kila mara walimtazama kwa makini mtu huyu, na kufikiri kuwa maneno kama hayo ndiyo ambayo yangesemwa na Kristo.TVV 450.1

  Akianzia kwa Musa, aliye Mwanzo wa unabii wa Biblia, Kristo alifafanua mambo yote katika Maandiko yaliyomhusu Yeye Mwenyewe. Kama angalijijulisha kwao tangu mwanzo, wasingehangaika na haja ya maelezo zaidi. Lakini ilikuwa lazima kwanza waelewe mifano na unabii wa Agano la Kale. Maana kwa hayo ndiyo imani yao ithibitike. Kristo hakufanya muujiza wo wote kuwasadikisha; kazi yake ilikuwa kuyaelezea Maandiko kwanza. Aliwafunulia kutoka kwa manabii kwamba kifo chake kilikuwa ndicho ushahidi wa dhati kwa imani yao.TVV 450.2

  Yesu alionyesha umuhimu wa Agano la Kale kama shahidi kwa kazi yake. Mwokozi anafunuliwa katika Agano la Kale wazi sawa kama katika Agano Jipya. Nuru kutoka katika unabii wa kale, hudhihirisha maisha ya Kristo na mafundisho ya Agano Jipya, kwa wazi na dhahiri. Uthibitisho wa dhati kuliko miujiza ya Kristo hupatikana katika kulinganisha unabii wa Agano la Kale na historia ya Agano Jipya.TVV 450.3

  Matazamio ya wanafunzi juu ya Masihi atakayetawala kwa mamlaka ya kifalme kama watu wanavyotamani yalikuwa yamepotoshwa. Wanafunzi wake lazima waelewe kikombe cha mateso alichopaswa kukinywea. Aliwaonyesha kuwa pambano hili la kutisha lilikuwa ni kutimizwa kwa agano lililotolewa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia. Kristo budi afe, sawa na kila mwenye dhambi atakavyokufa kama akidumu dhambini. Yote lazima yawe hivyo, lakini si katika kushindwa, bali katika ushindi wa utukufu. Yesu aliwaambia kuwa kila juhudi lazima ifanyike ili kuuokoa ulimwengu kutoka dhambini. Wafuasi wake lazima waishi kama alivyoishi yeye, na kutenda kazi kama alivyotenda kwa juhudi thabiti.TVV 450.4

  Hivyo Kristo aliwaeleza wanafunzi wake ili wapate kuyaelewa Maandiko. Alipokuwa akiwaambia juu yo kuangamizwa kwa Yerusalemu, waliutazama mji kwa huzuni. Lakini hata hivyo hawakufahamu mtu wanayesafiri naye ni nani, maana Kristo alijizungumzia kana kwamba ni mtu mwingine. Alitembea kwa uangalifu sana katika njia ya mawe kama wao, hapa na pale akisimama kupumzika kidogo.TVV 451.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents