Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dhoruba mioyoni mwa wanafunzi

    Siku hiyo tukufu sana ilikuwa imewajaza wanafunzi matumaini makuu, lakini walikuwa wameisahau kabisa. Mafikara yao yalikuwa ya mashaka tu na hoja zisizokuwa na sababu, kuwa Bwana angewapa kitu kingine cha kuwatuliza. Mungu mara nyingi hufanya hivi wakati watu wanapojisumbua na kujitia wenyewe kubeba mizigo isiyokuwa ya lazima. Wanafunzi haikuwapasa kujisumbua. Hatari ilikuwa ikiwajia karibuni.TVV 208.1

    Tufani ilikuwa ikiwakabili, lakini hawakuwa tayari kukutana nayo. Hatari hiyo ilikuwa jambo la tofauti kinyume cha mawazo yao, nayo ilikuwa tufani, ambayo ilipowatukia waliogopa. Hapo walisahau chuki yao, kutoamini kwao na kutosubiri kwao. Wakajitahidi, ili wasizame. Katika wakati wa kawaida safari hiyo ilikuwa ikichukua masaa machache tu, lakini sasa waliokotwa na kupelekwa mbali na kivuko chao. Mpaka kwenye kesha la nne walikuwa wakihangaika tu na makasia. Ndipo wachovu hawa walikata tamaa ya kuokoka. Walitamani Mwalimu wao, angekuwako.TVV 208.2

    Watu waliokuwa pwani waliwaona watu hao wakishindana na tufani. kwa macho yenye huruma sana Yesu aliiangalia mashua hii isumbukayo katika tufani, na watu waliomo humo, maana watakuwa nuru ya ulimwengu, waliomo humo, maana watakuwa nuru ya ulimwengu. Roho zao zilipotulia na mawazo mabovu yalipowatoka, ndipo waliomba msaada, nao wakapata.TVV 208.3

    Walipoona kuwa sasa wameangamia, ndipo umeme uliopomulika, waliona kitu kigeni, cha ajabu, kikitembea juu ya maji kinawakaribia. Aliyekuja kuwasaidia, wao walimhesabu kama adui wao. Hofu ikawajaa. Mikono yao yenye nguvu ikalegea. Mashua ikayumba kwa mawimbi. Macho yote yakamwelekea kiumbe huyu anayetembea juu ya maji.TVV 208.4

    Walifikiri kuwa ni pepo ambaye anakuja kuwaangamiza. Kwa hiyo walipiga kelele kwa hofu. Yesu aliendelea kama kwamba anataka kuwapita, lakini walimtambua, hivyo wakataka msaada kwake. Sauti yake ikawatuliza. Alisema: “Ni mimi, msiogope.”TVV 208.5

    Mara moja walipohakikisha kuwa ni yeye, Petro alisema, “Bwana, ukiwa ni wewe, niamuru nije kwako nikitembea majini.” Yesu akasema, “Njoo.”TVV 208.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents