Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kweli haikukubalika

  Wakati makutano yalipofuata mambo ya Yesu, na kulishwa chakula, sauti zao zilisikika zikiimba na kumsifu Yesu kwa hayo aliyowatendea, lakini ukweli uliposemwa na kudhihirisha kasoro zao na dhambi zao, walimgeuzia migongo yao, na kuisukumia kweli mbali.TVV 217.3

  Watu hao walipokwenda zao na kuiacha kweli, hali nyingine ya tofauti na ile ya kwanza iliwaongoza. Hawakuona faida yoyote juu ya yesu, ambaye kwanza alikuwa akiwapendeza sana. Waliyatafsiri maneno yake kinyume cha yalivyokuwa. Wakagombana kuhusu hali yake, wakikusanya mambo mbalimbali ya kumwendea kinyume. Mambo hayo ya uongo yalishindiliwa sana, hata akaonekana kuwa hafai kuishi.TVV 217.4

  Maneno yalienea kwa haraka sana, hata ikasemwa kuwa ametamka mwenyewe kuwa siye Masihi. Hivyo katika Galilaya habari kama hizo zikawa kikwazo kikuu kwake, kama ilivyokuwa katika Uyahudi. Waisraeli walimkataa Mwokozi wao kwa sababu walitamani chakula kiharibikacho, sicho kidumucho hata uzima wa milele.TVV 217.5

  Kwa masikitiko makubwa, Yesu aliona kuwa wale waliokuwa wanafuzi wake wakirudi nyuma. Huruma zake hazikujaliwa, upendo wake umedharauliwa, wokovu wake umekataliwa. Jambo hili lilimsikitisha mno. hali kama hii ijimfanya kuwa, mtu wa huzuni, ajuaye sikitiko. “IsayaTVV 217.6

  Bila kujaribu kuwazuia wale waliokuwa wakiondoka, yesu aliwageukia wale mitume kumi na wawili, akasema, “Ninyi pia manataka kuongoka”.TVV 217.7

  Petro alijibu akimwuliza hivi, “Bwana twende kwa nani? Wewe ndiwe una uzima wa milele. Nasi tumeamini kwa hakika kuwa wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu aliye hai”.TVV 218.1

  “Twende kwa nani? “Wanafunzi wamepata amani na utulivu wa kweli, tangu walipomwamnini Kristo, kuliko walivyokuwa hapo mwanzo. Watawezaje kwenda kwenye mizaha, watu watendao mabaya?TVV 218.2

  “Twende kwa nani” Katika giza la kutokuamini, katika uovu wa dunia? Petro alieleza imani ya wanafunzi wote waliyokuwa nayo. “Wewe ndiwe Kristo” Kuachana katika bahari yenye dhoruba.TVV 218.3

  Kila neno tendo la Yesu lilikuwa na kusudi maalumu, katika mpango wa wokovu. Wakati sisi tusipofahamu njia za Mungu, ni vigumu kufahamu mema yote Mungu anayoyaweka kwa ajili ya watu wake. Mtu anayeishi karibu na Yesu atafahamu huruma zake na kuona makusudi ya moyo wake.TVV 218.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents