Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    52 — Mchungaji, Mungu

    “Mimi ndimi Mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Yohana 10:11.TVV 271.1

    Yesu alipata usikizi kwa watu wake kwa njia ya kuwapa mambo wanayoyazoea kufanya. Kwa watu waliomwamini aliwatolea mfano wa Mchungaji mwema. Hakuna mfano uliojulikana kwa wasikilizaji wake zaidi ya huu. Wakikumbuka fundisho lake, wanafunzi wake wataweza kuona jinsi Kristo anavyofanana na kila mchungaji, mwaminifu na wao kama kondoo wasioweza kujisaidia.TVV 271.2

    Mafarisayo walikuwa wamemfukuza mtu mmoja, aliyemshuhudia Kristo. Walimwondoa mtu, ambaye Mchungaji halisi alikuwa akimtafuta kwa njia hii walijionyesha kuwa ni wachungaji wasiofaa kitu. Na sasa Yesu alijitambulisha kuwa mchungaji halisi wa kundi la Bwana.TVV 271.3

    “Asiyeingia kwa mlango, lakini akiingia kwa kupitia mahali pengine ni mwizi na mnyanganyi. Lakini aingiaye kwa mlango ni mchungaji wa kondoo.” Mafarisayo walipowaza mioyoni inwao maana yake, Yesu aliwaambia waziwazi: “Mimi ndiye mlango wa kondoo, mtu akiingia kwangu atakuwa salama, ataingia na kutoka na kupata malisho. Nimekuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”TVV 271.4

    Kristo ndiye mlango wa zizi la Mungu. Watu wake tangu zamani wamepata kuingia. Mifano yake ikitiwa weusi, na mafundisho yake yakipotoshwa, hata hivyo wamemtazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu. Yohana 1:29. Ibada na kawaida vilikusudiwa kuwaletea watu matumaini na kuwapa watu haki na utulivu pamoja na Mungu. Lakini waliovumbua mambo mengine mbali na Kristo, ili kuwaingiza zizini, ni wezi na wanyang’anyi.TVV 271.5

    Makuhani, wakuu, waandishi na mafarisayo, wameharibu mfano uliowekwa ili kuwaongoza, pamoja na uchungaji wa kweli na maji yaliyo hai. Maandiko huwataja hawa kuwa: “Wagonjwa hawakuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala kuwarudisha waliofukuzwa, wala kutafuta waliopotea, bali kwa nguvu na ukali mmewatawala.” Ezekiel 34:4.TVV 272.1

    Kila taifa Umekuwa na walimu wake, na dini yake pamoja na matoleo yake ya dini, ambayo ni mbali kabisa na ukombozi wa Kristo, wamekuwa wakigeuza nyuso zao kinyume na Mungu na kuwajaza watu na hofu tu. Watu mamilioni wanazo dini za uongo, ambazo haziwaletei furaha, ila huwaletea giza na hofu za siku za usoni. Injili ya neema ya Mungu peke yake ndiyo huwainua watu na kuwaletea utulivu kuliko kitu kinginecho. Anayewageuzia watu mbali na Kristo, huwageuzia watu mbali na maendeleo yoyote na kuwaondoa katika njia ya kupata utukufu na uzima. Mtu kama huyu ni mwizi na mnyang’anyi.TVV 272.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents