Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mbingu yatia Sahihi

    Maneno hayo yalisemwa ili kuimarisha imani ya wale walioona jambo hilo, na kumtia moyo Mwokozi kwa kazi yake. Ingawa uovu wa dhambi ya ulimwengu uliwekwa juu ya Kristo, ingawa amejidhili kiasi hicho, sauti kutoka mbinguni ilimtaja kuwa Mwana wa Mungu wa milele.TVV 55.1

    Yohana alishangaa sana. Kwa vile utukufu wa Mungu ulivyomzunguka Yesu, na sauti kutoka mbinguni ilisikika. Yohana alijua kuwa huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu ambaye amembatiza. Halafu akinyosha mikono yake kuelekea kwa Yesu, alipaza sauti na kusema, “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana 1:29. Hakuna mtu, hata msemaji mwenyewe, aliyefahamu umuhimu wa maneno hayo, yaani “Mwanakondoo wa Mungu. Watu wengi wa wana wa Israeli walihesabu kafara walizokuwa wakitoa, kama wakafiri wanavyozihesabu, yaani ni kafara za kumfurahisha Mungu ili awajalie. Mungu alikusudia kuwafundisha kuwa kutokana na kipaji chake cha upendo waweze kupatanishwa kwake.TVV 55.2

    Maneno yaliyosemwa kwa Yesu, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ninayependezwa naye,” yaliwakumbatia watu wote kwa Mungu. Sote tukiwa na dhambi na takataka zote, Mungu hatutupi kama vitu ovyo. Ametupokea kwa njia ya Mwana wake. Waefeso 1:6.TVV 55.3

    Utukufu uliomwangukia Kristo, ilikuwa thibitisho la upendo wa Mungu kwetu. Hutuambia uwezo wa maombi, jinsi maombi ya wanadamu yanavyofika katika sikio la Mungu, na sala zetu zinavyokubalika katika mbingu. Nchi ilitengwa na mbingu kwa ajili ya dhambi, lakini Yesu ameiunganisha tena kwa njia ya sala, ya utukufu. Nuru iliyomwangukia Yesu, hata sisi itatuangukia tunapoomba ili tushinde majaribu. Sauti iliyosema kwa Yesu, husema kwa kila mwamini, kwamba, ‘Huyu ni mtoto wangu mpendwa, ninayependezwa naye.”TVV 55.4

    Mwokozi wetu amefungua njia, ili mtu mwenye dhambi hasa, maskini, adharauliwaye, apate kamfikia Baba. Wote waweze kupata makao katika yale ambayo Yesu amekwenda kuwaandalia.TVV 55.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents