Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Yesu alivyowaheshimu wote

    Kristo alikuta dini imezungushiwa ua, kama ni kitu kisichotaka kuonekana katika maisha ya kila siku. Ua huo yeye aliubomoa. Badala ya kujifungia ndani ya chumba ya kujitenga na watu, ili kuonyesha tabia ya mbinguni, alifanya kazi ya kusaidia watu. Alifundisha kuwa dini siyo kitu cha muda fulani, na wakati fulani tu, ila ni huduma ya wakati wote. Jambo hili lilikuwa kemeo kubwa kwa walimu wa Kiyahudi na mafarisayo. Jambo hili lilionyesha kuwa dini yao ni mfano tu, ilikuwa kinyume cha utauwa. Liliamsha uadui, kwa vile walivyotaka kuwalazimisha watu kufuata desturi zao.TVV 42.3

    Yesu alikuwa na fedha kidogo tu, kwa hiyo hakuwa na kitu cha kutoa. Kwa hiyo kila mara alikataa chakula ili kiwasaidie wahitaji zaidi yake. Wakati ndugu zake walipowakemea maskini, yeye aliwafariji na kuwatia shime. Kwa wahitaji aliwapa ingawa kikombe cha maji baridi, na chakula kidogo alicho nacho.TVV 42.4

    Mambo kama hayo yaliwachukiza ndugu zake. Kwa kuwa walikuwa wakubwa kuliko yeye, waliona kuwa ingempasa Yesu kuwaheshimu na kuwatii. Walimlaumu kwa kujikuza kuliko wote hata na walimu wake pia. Kwamba anajitukuza kupita makuhani, hata kupita watawala. Mara kwa mara walimtisha, lakini aliwapita akiwasomea Maandiko, na kuyafanya kuwa ndiyo mwongozo wake.TVV 42.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents