Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wakati Hali ya Baadaye ya Ulimwengu ilipotetemeka kwenye Mizani

    Yesu akigeuka, kwenda mahali pale pa kuombea alianguka kifudifudi. Hali ya Ubinadamu ya Mwana wa Mungu ilitetemeka katika saa ile ya majaribu. Saa ya kutisha ya kuamua, hali ya baadaye ya ulimwengu ilikuwa imewadia. Hali ya baadaye ya jamii ya walimwengu ilitetemeka katika mizani. Kristo angeweza hata wakati huu akatae kukinywea kikombe kilichogawiwa kwa Mwanadamu mwenye hatia. Angeweza kujipangusa jasho lake la damu na kumwacha mwanadamu kupotea katika uovu wake. Angeweza kusema, muwache mwenye dhambi apokee adhabu ya dhambi yake, mimi nitarudi kwa Baba yangu. Je, asiye na hatia ateseke kwa ajili ya matokeo ya laana ya dhambi, kuwaokoa wenye hatia? “Baba yangu, uniondolee kikombe hiki; walakini si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.”TVV 389.2

    Mara tatu alinywea kwa hofu asikaribie hatua ya mwisho ya kukamilisha kafara. Lakini sasa anaona kuwa jamii ya mwanadamu haina msaada. Anaona nguvu za dhambi. Misiba ya ulimwengu unaoangamia iliinuka mbele yake, anaona ajali yake iliyo karibu sana, naye anafanya uamuzi. Atamwokoa mwanadamu kwa gharama yo yote ile. Ametoka mbinguni ili kuja kuiokoa dunia moja iliyo anguka katika uasi. Na hawezi kurudi nyuma kwa utume wake. Baada ya kuamua, alianguka chini kama mfu. Wanafunzi wake wako wapi sasa wapate kumwinua Bwana wao aliyezimia? Mwokozi alikanyaga shinikizo peke yake, wala hakuna mtu aliyekuwa pamoja naye. (Tazama Isaya 63:3).TVV 389.3

    Lakini Mungu aliteseka na Mwanaye. Malaika waliona masumbuko yake. Mbinguni kulinyamaza kimya. Hakuna sauti ya kinubi iliyosikika huko. Malaika wakinyamaza kwa huzuni, walimwangalia Baba akiondoa miali yake ya nuru upendo na utukufu kutoka kwa Mwanawe mpendwa.TVV 389.4

    Shetani na jeshi lake ovu waliangalia kwa makini. Maombi ya Kristo aliyoomba mara tatu kuhusu kikombe yatajibiwaje? Wakati huu wa kutisha, wakati kikombe kile cha siri kilipotingishwa mkononi mwa mteswa, yule malaika mkuu anayesimama mbele za Mungu, alikuja na kuwa kando ya Kristo. Malaika hakuja kumwondolea Kristo kikombe mkononi, bali alikuja kumhakikishia kuwa Baba yake bado anampenda. Alimhakikishia kwamba kifo chake kitamshinda Shetani kabisa, na kwamba ufalme wa ulimwengu huu watapewa watakatifu wa Mwenyezi Mungu, na alimwambia kwamba ataona umati wa watu wa ulimwengu wakiokolewa, na kuokolewa milele.TVV 390.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents