Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    83 — Kutembea Kwenda Emau

    Jioni ya siku ile ile ya kufufuka kwake Kristo, wanafunzi wawili walikuwa njiani wakienda Emau mji mdogo umbali wa maili nane kutoka Yerusalemu. Wanafunzi hawa waliokuwa wamekuja kuadhimisha Pasaka, walikuwa na hali ya wasiwasi mkubwa kuhusu mambo yaliyokuwa yametokea. Walikuwa wamesikia habari za mwili wa Kristo kuondolewa kaburini, pia habari zingine kutoka kwa wanawake waliosema wamewaona malaika na kwamba wamekutana na Yesu. Na sasa wakiwa njiani kurudi nyumbani walikuwa wakiongea matukio ya kesi na kusulibishwa kwa Kristo. Walikuwa hawajapata kukatishwa tamaa hivyo.TVV 449.1

    Katika kwenda kwao walikutana na kufuatana na mtu wasiyemjua, na kwa vile walikuwa na wasiwasi sana hawakushughulika kumhoji. Waliendelea kuzungumzia yaliyokuwa mioyoni mwao na mafundisho yaliyotolewa na Kristo, ambayo walionekana kutofahamu. Yesu alitamani kuwafaariji. Alielewa utata waliokuwa nao mawazoni, na shauku lililokuwa mioyoni mwao “Mtu huyu, Aliyekabili kudhalalishwa hivyo anaweza akawa ndiye Kristo?” Wakalia. Yesu alitamani kuyafuta machozi yao, na kuwajaza furaha na shangwe. Lakini lazima kwanza awape fundisho ambalo hawatalisahau.TVV 449.2

    “Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayoseme-zana hivi mnapotembea? Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata hujui yaliyotukia humo siku hizi? Wakamweleza huzuni yao juu ya Bwana wao, “aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; lakini “wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha.” Kwa midomo iliyotetemeka wakaongeza, “Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo.” Ni ajabu kwamba hawakukumbuka maneno ya Kristo, na kwamba Alikuwa Ametabiri kuwa siku ya tatu Atafufuka. Makuhani na wakubwa hawakusahau!TVV 449.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents