Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    66 — Kristo Akabiliana na Adui Zake

    Makuhani na wazee hawakuweza kukanusha madai ya Kristo, ila tu walinuia kumtega. Walimtumia mijasusi “waliojifanya kuwa waaminifu kwake, ili wapate kumka-mata katika maneno yake, na kumshitaki kwa watawala.” Vijana hao wenye juhudi walifuatana na wafuasi wa Herode kusudi wasikie maneno yake wapate kumnasa na kumshitaki.TVV 337.1

    Mafarisayo waliudhiwa na kodi za Warumi wakidai kuwa kulipa kodi ni kinyume cha sheria ya Mungu. Sasa majasusi walimjia Yesu wakijifanya wanataka kujua wajibu wao, wakisema: “Bwana, twajua kuwa wewe hufundisha ukweli mtupu, wala hujali cheo cha mtu, ila hufundisha sheria ya Mungu tu: Je, ni halali kumlipa Kaisari kodi kwa Kaisari?”TVV 337.2

    Wale waliomwuliza Yesu swali hilo walidhani kuwa wameficha kusudi lao, lakini Yesu alisoma nia yao kana kwamba ni kitabu. Akasema: “Mbona mnanijaribu?” Alisema hayo kuonyesha kuwa anafahamu nia yao. Walikuwa bado wangali katika mtataniko, aliposema: “Nionyesheni dinari.” Walimletea. Naye aliwauliza: “Sanamu hii ni ya nani?” Wakasema, “Ni ya Kaisari.” Yesu akisonda dinari hiyo alisema: “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.”TVV 337.3

    Wapelelezi walijiona kuwa duni katika mtego wao na kushindwa. Ufasaha wa majibu ya maswali yao uliwafanya wasiwe na la kusema zaidi. Majibu ya Kristo hayakuwa ya kupiga chenga, bali majibu adilifu kwa maswali yao. Akishikilia dinari ya Kirumi mkononi aliwaambia kuwa kwa kuwa wanaishi chini ya ulinzi wa Warumi, ni haki kabisa kulipa kodi kwao. Lakini wakiwa chini ya sheria ya Warumi lazima utii wao kwanza uwe kwa Mungu.TVV 337.4

    Kama Wayahudi kwa uaminifu wangalitimiza wajibu wao kwa Mungu, wasingalitawaliwa na watu wa mataifa mengine. Bendera ya Warumi isingalipepea katika Yerusalemu; wala mtawala wa Kirumi asingelitawala humo.TVV 337.5

    Mafarisayo walishangazwa na majibu ya Yesu. Hakuwakemea tu bali alieleza kanuni zinazohusu wajibu wa watu kwa Mungu wao na wajibu wao kwa serikali inayotawala. Ingawa wengi hawakuridhika, lakini waliona kanuni ilivyo kwa majibu ya maswaii yao. Walishangazwa kwa uwezo wa Kristo kwa kujibu.TVV 338.1

    Haukupita muda mara baada ya Mafarisayo kunyamazishwa Masadukayo nao wakajitokeza na maswali ya ujanja. Ingawa hawakumwamini Kristo kwa ujumla, lakini baadhi yao walikuwako waaminifu katika mafundisho ya Kristo. Masadukayo walikiri kuwa Wanaamini sehemu kubwa ya Maandiko Matakatifu, lakini kimaisha walikuwa wenye mashaka na wapenda utajiri.TVV 338.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents