Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Matumaini ya ubinafsi hayakutimiz.wa

    Yesu alifanya kazi ile unabii ulivyosema kuwa Masihi ataifanya, lakini watu hawakuona kazi ambayo matumaini yao ya ubinafsi yalitazamia kuona. Siku zile za Musa Waisraeli walikula mana miaka arobaini, ambayo ilikuwa mibaraka ya Masihi. Kwa nini Yesu hangeweza kuwapa watu wake afya, nguvu, na utajiri, na kuwafungua watoke katika utumwa na kuwainua wawe watawala? Anadai kuwa alitumwa kutoka kwa Mungu, huku anakataa kuwa mfalme wa Waisraeli. Jambo hili lilikuwa fumbo, ambalo hawakulielewa. Je, hawezi kuthibitisha madai yake kwa sababu anaona mashaka kuhusu Uungu wake na kazi yake? Nusu ya watu walidhihaki swali la Marabi, kwamba “unatuonyesha ishara gani ili tuone na kukuamini Unafanya nini? Baba zetu waliila mana jangwani, kama ilivyoandikwa: Aliwapa chakula kutoka mbinguni wakala.”TVV 212.2

    “Kisha Yesu akasema: Amini, Amim nawaambiem, Musa hakuwapa mkate ule kutoka mbinguni.” Mtoaji wa mkate huo alikuwa anasimama katikati yao. Kristo mwenyewe ndiye aliyekuwa akiwaongoza Waisraeli jangwani na kuwalisha mkate huo kila siku kutoka mbinguni. Chakula kile kilikuwa mfano wa chakula cha kweli cha mbinguni. Chakula cha kweli ni ile mana iliayo uzima, ambayo ni chakula cha kiroho. Maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.TVV 212.3

    Hata hivyo wangali wakidhani kuwa ni chakula cna kawaida, kwa hiyo wengine waliuliza: “Bwana, utupatie chakula hicho. Ndipo Yesu akasema dhahiri: “Mimi ndimi mkate wa uzima.”TVV 212.4

    Musa alikuwa amesema: “Mtu hataishi kwa mkate peke yake, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana.” Torati 8:3. Na Yeremia alikuwa ameandika: “Maneno yako yalionekana kwangu nikayala, na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.” Yeremia 15:16. Mafundisho ya manabii yalidhihirisha mambo ya kiroho kuhusu mwujiza wa mikate. kama wasikilizaj: wa kristo katika sinagogi wangalifahamu maandiko, wangalifahamu maneno yake pia. “Mimi ni chakula cha uzima.” Kama vile makutano walivyopokea chakula alichowapa siku nyingine, ndivyo wangalipokea kwa Kristo maneno ya uzima, yawezayo kuwapa uwezo wa kupata uzima. Yesu alisema: “Yeye ajaye kwangu hataona kiu kamwe,” Tena aliongeza kusema: “Ninyi mmeniona, wala hamkuniamini.”TVV 212.5

    Wamemwona kristo kwa kushuhudiwa na Roho mtakatifu, na kwa mafunuo ya Mungu katika mioyo yao. Ushahidi wa kweli zaidi ni ule wa kuwa kati yao siku kwa siku na kuona uwezo na nguvu zake, walakini bado wakawa wanataka ishara yake. Kama hawakuaminishwa kwa yale waliyoona na kusikia, ilikuwa kazi bure kuzidi kuwaonyesha mambo zaidi, wangalipata udhuru zaidi wa kutokuamini, na hata kama wangepata uthibitisho mkubwa kadiri gani, wangalidumu kutokuamini.TVV 213.1

    Mara nyingine tena Kristo aliwasihi watu hao wenye shingo ngumu: “Ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.” Wote wanaompokea Kristo kwa imani, asema, watapata uzima wa milele. Hakuna tena watu kulalamika katika mashaka na kutokuwa na matumaini. Yesu alisema: “Mapenzi yake aliyenipeleka ni haya: Mtu akimwona Mwana, na kumwamini anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.”TVV 213.2

    Lakini viongozi walichukizwa, wakasema: “je, huyu siye Yesu mwana wa Yususu, ambavyo tunawafahamu baba yake na mama yake? Anawezaje kusema kuwa, nimeshuka kutoka mbinguni?” Wakasema kwa dhihaka kuwa ni mtu aliyezaliwa katika hali ya kimaskini tu, wakisema kuwa ni mwana wa seremala, asiyekuwa na elimu. Walipoona uzazi wake ni wa ajali wakamtilia shaka.TVV 213.3

    Yesu hakujaribu kuelezea kuhusu uzazi wake wa ajabu, wala hakuwajibu swali lao juu ya jinsi alivyovuka bahari. Alijifanya kuwa hana utukufu, akawa kama mtumwa. Lakini maneno yake yalidhihirisha tabia yake ya kweli.TVV 213.4

    Udhalimu wa Mafarisayo ulitokana na ukaidi wa mioyo yao. Kila neno na tendo la Yesu liliamsha upinzani kwao, maana roho waliyopendelea kuwa nayo haikuwa roho safi!TVV 213.5

    Yesu alisema: “Hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu .... Imeandikwa katika manabii, wote watafundishwa na Mungu. Kila mtu aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu.” Hakuna watakaokuja kwa Kristo isipokuwa ni wale waliokubali mvuto wa Baba wa upendo. Lakini Mungu huwavuta watu wote, isipokuwa ni wale wanaopinga mvuto wake ndio hawatakuja kwake. Waliojifunza kwa Mungu huja kwa Mwana wake, na kwa Yesu wa Nazareti watamtambua yule ambaye Yesu humwita kuwa Baba.TVV 213.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents