Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Petro Alirudishwa Katika Hali ya Kutumainika

    Kristo alihitaji kutoa fundisho jingine. Kwa Petro kumkana Bwana wake ilikuwa aibu na kinyume kabisa na madai yake ya awali ya kuwa mtiifu. Alikuwa amemdhalalisha Bwana wake, na ndugu zake hawakudhani kuwa Petro hatarudia kuwa mmoja wao tena. Hata yeye mwenyewe pia aliona kuwa amepoteza imani yake. Yampasa adhihirishe mbele zao ushahidi wa toba yake. Bila hivyo dhambi yake ingeadhiri mvuto wake kama mhudumu wa Kristo. Mwokozi alimpa nafasi tena ya kurudisha hadhi yake mbele ya ndugu zake, kadri iwezekanavyo aondoe aibu aliyoleta kwa kazi ya injili. Hapa liko fundisho kwa wafuasi wote wa Kristo. Dhambi za siri lazima ziungamwe kwa Mungu kwa siri; bali kwa dhambi za wazi toba ya wazi huhitajika. Dhambi ya mwanafunzi humfanya Shetani ashinde na roho zenye kusita kujikwaa. Kwa kuonyesha ushahidi wa toba mwanafunzi ataondoa aibu hii.TVV 458.3

    Wakati Kristo na wanafunzi walipokuwa wakila pamoja, Mwokozi akamwambia Petro,” Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?” akiwa na maana ya wanafunzi wenzake. Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana kondoo wangu. Hakukuwa na msisitizo kuwa upendo wake ulikuwa mkuu kuliko ule wa wenzake.TVV 458.4

    Tena Mwokozi akarudia mtihani, “Simoni wa Yohana, wanipenda? Jibu la pili lilikuwa kama lile la kwanza, lisilokuwa na kujitapa; “Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.” Yesu “Akamwambia, chunga kondoo zangu.”TVV 459.1

    Kwa mara nyingine tena Mwokozi akauliza swali la mtihani; “Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro akahuzunika. Alijua kuwa Bwana wake alikuwa na sababu ya kutomwamini, na kwa moyo uliouma akajibu; “Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia tena, “Lisha kondo zangu.TVV 459.2

    Petro alikuwa amemkana wazi Bwana wake mara tatu, na mara tatu Yesu alimsonga na lile swali lilichoma moyo wake uliojeruhiwa kama mshale. Mbele ya kusanyiko la wanafunzi Yesu alifunua kina cha toba ya Petro na kuonye-sha jinsi yule mwanafunzi jeuri na mwenye kujitapa alivyokuwa ameshushwa.TVV 459.3

    Muda kitambo kabla ya kuanguka kwa Petro, Yesu alikuwa amemwambia, “Nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako,” (Luka 22:32). Badiliko katika Petro lilikuwa dhahiri. Kwa sababu ya kunyenyekea na toba, Petro alijiandaa vizuri zaidi kuliko hapo awali kama mchungaji wa kundi.TVV 459.4

    Kazi ya kwanza Kristo aliyomkabidhi Petro ilikuwa kulisha “wana kondoo” kuhudumia wale waliokuwa wachanga katika imani, kuwafundisha wasiojua, kuyafungua Maandiko kwao na kuwaelimisha wafae katika huduma ya Kristo. Mateso yake pamoja na toba vilikuwa vimemwandaa kwa ajili ya kazi.TVV 459.5

    Kabla ya anguko lake, Petro siku zote alikuwa tayari kuwasahihisha wengine na kutoa maoni yake. Lakini Petro mwongofu alikuwa tofauti kabisa. Alidumisha mwamko wake wa kwanza, lakini neema ya Kristo ilirekebisha juhudi zake. Sasa aliweza kuwalisha wana kondoo pamoja pia na kondoo wa kundi la Kristo.TVV 459.6

    Namna ya Mwokozi ya kumshughulikia Petro iliwafunza wanafunzi kumkabili mkosaji kwa uvumilivu, huruma, na upendo unaosamehe. Akikumbuka udhaifu wake mwenyewe, Petro angeshughulikia kundi lake kwa upole jinsi Kristo alimshughulikia yeye.TVV 459.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents