Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    82 — “Mama Unalilia Nini?

    Katika siku ya kwanza ya juma, asubuhi na mapema wanawake waliokuwa wamesimama kando ya msalaba, walikwenda kaburini kuupaka mwili wa Mwokozi marhamu. Hawakuwa wanafikiria juu ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Jua la matumaini yao lilikuwa limekuchwa. Wala hawakukumbuka maneno yake kuwa, “lakini mimi nitawaona tena.” Yohana 16:22.TVV 445.1

    Bila hata ya kufahamu kilichokuwa kinatendeka walilikaribia bustani, huku wakisema: “Ni nani atakayetuviringishia lile jiwe mlangoni pa kaburi?” Lo, tazama mbingu zikang’aa kwa utukufu. Nchi ikatetemeka. Jiwe lile kubwa lilikuwa limeviringishwa mbali, na kaburi lililokuwa tupu!TVV 445.2

    Mariamu Magdalena ndiye aliyefika kaburini mara ya kwanza, na walipoona jiwe limevingirishwa, aliharakisha kwenda kuwaambia wanafunzi, habari hizo. Wakati huo pia wale wanawake wengine wakafika. Nuru ilikuwa iking’aa kaburini, lakini mwili wa Yesu haukuwemo.TVV 445.3

    Walipokuwa wakizungukazunguka hapo, ghafula wakajikuta kuwa hawako peke yao, kijana mmoja mwenye mavazi meupe alikuwa ameketi kando ya kaburi. Kumbe ni malaika aliyelivingirisha lile jiwe. Alikuwa na umbo la kibinadamu ili asiwaogopeshe watu hawa. Hata hivyo kando yake utukufu wa mbinguni ulikuwa uking’aa, na wale Wanawake waliogopa. Malaika akajibu, akawaambia: “Msiogope, ninyi, kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka, kama alivyosema. Njoni mpatazame mahali alipolazwa. Ninyi nendeni, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu.”TVV 445.4

    Walipoangalia kaburini malaika mwingine mwenye sura ya kibinadamu, alisema: “Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, akasema: Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu.TVV 445.5

    Wanawake wale wakakumbuka sasa, Alisema kuwa atafufuka tena! Ni siku ya furaha kiasi gani kwa ulimwengu! “Wakaondoka upesi kutoka kaburini., kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Mariamu alikuwa hajasikia habari hizi njema. Aliwaendea Petro na Yohana na habari za huzuni kwamba wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.” Wanafunzi wakakimbia kwenda kaburini wakaona vitambaa na leso ila hawakumwona Bwana wao. Hata hivyo huu ulikuwa ushahidi kuwa Amefufuka. Sanda yake haikuwa imetupwa ovyo, bali ilikunjwa na kuwekwa vizuri. Yohana “akaona akaamini.” Sasa akakumbuka maneno ya Mwokozi alivyotabiri kuwa atafufuka.TVV 446.1

    Kristo Mwenyewe aliweka sanda ile kwa hali ya mpangilio hivyo. Malaika mwenye uwezo alipokuja kutoka mbinguni na hakulivingirisha jiwe, malaika mwingine aliingia na kufungua sanda mwili wa Yesu. Lakini ni mikono ya Mwokozi mwenyewe ndiyo iliikunja sanda na kuiweka katika hali ya safi. Kwake yeye ambaye hata hupanga nyota zote na kuongoza mwendo wao hakuna kisicho na muhimu.TVV 446.2

    Mariamu alikuwa amewafuata Yohana na Petro mpaka kaburini; waliporudi Yerusalemu, yeye alibakia kaburini. Huzuni ilizidi. Alipotazama ndani ya kaburi aliwaona wote malaika wawili wakiwa wameketi humo, mmoja upande wakichwa na mwingine upande wa miguuni Yesu alipokuwa amelazwa. Wakamwuliza “Mama unalilia nini? Akawaambia “Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.”TVV 446.3

    Kisha aligeuka ili kutafuta mtu wa kuuliza kile kilichoupata mwili wa Yesu. Sauti nyingine ikamwambia, “Mama unalilia nini.” Unamtafuta nani? Mariamu huku akitokwa na machozi akamwona mtu ambaye alidhani kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, “Bwana ikiwa umemchukua wewe uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.” Ikiwa kaburi hili la mtu tajiri halitakiwi kumzika Yesu, yeye atampatia mahali pa kuzikwa. Kulikuwa na kaburi ambalo sauti ya Yesu mwenyewe ililifanya tupu, kaburi ambamo Lazaro alikuwa amelazwa.TVV 446.4

    Lakini sasa kwa sauti yake iliyozoeleka Yesu alijibu “Mariamu”. Akigeuka alimwona Yesu aliye hai. Kwa shangwe akamrukia akitaka kumkumbatia miguu akasema: “Raboni! Lakini Kristo aliinua mikono yake akasema: “Usinishikilie” “kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie; Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” Mariamu akaenda zake akiwa na ujumbe wa nderemo.TVV 446.5

    Yesu alikataa kuheshimiwa na watu wake, kabla hajapaa kwenda mbinguni na kutoka kwa Baba mwenyewe apate uthibitisho kuwa kafara yake kwa ajili ya dhambi za wanadamu imetosha kabisa na kwamba kwa ajili ya damu yake wanadamu wote watapokea uzima wa milele. Baba akathibitisha agano lililofanywa na Kristo, kwamba atawapokea wanadamu wenye toba, na utii na kuwapenda kama anavyompenda Mwana wake. Uwezo wote mbinguni na duniani alipewa mkuu wa Uzima ili aweze kuwapa uwezo wake na utukufu wafuasi wake.TVV 447.1

    Wakati Mwokozi alipokuwa mbele ya Mungu, akipokea vipawa kwa ajili ya kanisa lake, wanafunzi walikuwa wakiomboleza na kulia. Siku ya mashangilio makuu mbinguni, kwao ilikuwa ni siku ya kiwewe na utata. Kutokuamini kwao ushuhuda wa wanawake kulidhihirisha jinsi imani yao ilivyokuwa imeshuka. Hawakuweza kuamini taarifa ile. Ilikuwa nzuri mno kuweza kuwa kweli walidhani. Waliishasikia dhana nyingi za Masadukayo kiasi kwamba hawakuweza kujua maana ya ufufuo kutoka kwa wafu.TVV 447.2

    Malaika waliwaambia wale “Lakini enendeni, zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya, huko mtamwona, kama alivyowaambia.” Ujumbe wa malaika hawa kwa wanafunzi ulipaswa kuwasadikisha juu ya ukweli wake. Maneno kama haya yangaliweza tu kuelea na wajumbe wa Bwana wao Aliyefufuka.TVV 447.3

    Tangu kifo cha Kristo, Petro alikuwa amelemewa na majuto makuu. Aibu ya kumkana Bwana wake ilikuwa daima mawazoni mwake. Alikuwa ameteseka sana kuliko wanafunzi wote. Kwake uthibitisho ulitolewa kuwa toba yake imekubalika. Alitajwa kwa jina.TVV 447.4

    Mariamu Magdalena alipowaambia wanafunzi kuwa amemwona Bwana, alirudia wito wa kukutana kule Galilaya. Tena ujumbe ulitumwa kwao mara ya tatu. Baada ya kupaa kwa Baba, Yesu aliwatokea wanawake wengine akawaambia: “Nendeni mkawaambie ndugu zangu, waende Galilaya huko watakutana nami.TVV 447.5

    Kazi ya Yesu ya kwanza baada ya kufufuka ilikuwa kuwadhihirishia wanafunzi wake juu ya upendo wake usiofifia na kuwajali kwake. Ataendelea kuwavuta kwake kwa kamba za upendo. Alisema; Nendeni mkawaambie ndugu zangu kuwa tukutane Garilaya.TVV 447.6

    Lakini hata wakati huu wanafunzi walikuwa bado wangali na utata na mashaka. Hata wakati wanawake walipowaambia; kwamba wamemwona Bwana, waliwadhania kuwa wameona mazingaombwe.TVV 448.1

    Taabu ilionekana kuongezeka juu ya taabu. Walikuwa wamemwona Bwana wao akifa; walijikuta wamepokonywa mwili wake; na walikuwa wameshitakiwa kwa kuiiba mwili wake kusudi kuwadanganya watu. Walikata tamaa kuwa kamwe hawataweza kusahihisha uongo huu uliokuwa unazagaa. Waliogopa uhasama wa makuhani na ghadhabu ya watu. Walitamani mno kuwepo Yesu.TVV 448.2

    Mara nyingi walirudiarudia maneno haya, “Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli.” Luka 24:21. Wakijisikia wapweke na wenye mashaka moyoni, walikutana pamoja katika chumba cha ghorofa, na kufunga milango kwa hofu kuwa yaliyompata Mwalimu wao mpendwa yangeweza kuwapata wakati wo wote ule.TVV 448.3

    Na kwa wakati wote wangekuwa na furaha katika kufahamu kuwa Mwokozi amefufuka. Watu wengi bado wanafanya kile walichokifanya wanafunzi hawa. Mwokozi yuko kando yao, lakini macho yao yaliyofumbwa na machozi hayamtambui. Anazungumza nao lakini hawaelewi.TVV 448.4

    “Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka. ” Usitazame kaburi lililotupu. Kutoka katika mioyo yenye furaha, kutoka katika midomo iliyoguswa na moto mtakatifu, hebu wimbo wa shangwe usikike, Kristo Amefufuka! Yu hai kutuombea.TVV 448.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents