Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mawazo ya Mungu yakalibisha tabia

  Mawazo yao kuhusu Mungu ndiyo yaliyokalibisha tabia zao. Kwa kuwa hawakuona kuwa Mungu hushugulika na watu, hata wao hawakushughulika kuhusu mtu na mtu. Wakikataa mvuto wa Roho Mtakatifu, walipungukiwa na nguvu zake katika kuongoza maisha yao. Walijivunia tu kuwa wao ni wa uzao wa Ibrahim, lakini hawakuwa na imani yake. Hawakuhangaika kuwafikiria wengine, ila waliishi maisha ya ubinafsi. Katika maneno na kazi zake Kristo alishuhudia uwezo wa Mungu wa kushughulikia watu kwa maisha ya baadaye, Mungu kama Baba wa watu wote. Akiwatunza kwa kila hali. Alifundisha kuwa Mungu huwavuvia watu kwa Roho wake Mtakatifu. Alionyesha makosa ya kutegemea uwezo wa mwanadamu kuleta mabadiliko ya tabia, ambayo ni kazi ya Roho wa Mungu.TVV 338.6

  Katika kutafuta majadiliano na Yesu Masadukayo walitumaini kumletea sifa mbaya, kama si kumlaumu. Walichagua kumwuliza swali kuhusu ufufuo wa wafu. Kama akikubaliana nao, atawaletea Mafarisayo machukizo. Lakini asipokubaliana nao, watayahesabu mafundisho yake kuwa ya ovyo. Masadukayo walidhani kuwa ikiwa mwili wa marehemu huwa katika hali yake ya kutokufa katika hali ile ile ya mtu hai, basi uwe na nyama na damu na uendelee katika umilele na hali ile iliyokatishwa katika ulimwengu huu. Mume na mke wataungana tena, na kutimiliza ndoa mambo yao yataendelea kama yalivyokuwa kabla ya mauti.TVV 339.1

  Katika kuwajibu Yesu alifunua pazia ili waone mambo ya mbele. Alisema: “Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.” Mathayo 22:30. Masadukayo walikuwa na makosa. Alisema: “Hamjui Maandiko, wala uwezo wa Mungu.” Hakusema kuwa ni wanafiki, ila wanakosea katika imani yao.TVV 339.2

  Alisema kuwa kutojua kwao Maandiko, pamoja na kutojua uwezo wa Mungu ndizo sababu za kutatanika katika imani na kuchanganyikiwa kwao. Kristo aliwataka wafungue mioyo yao na kusoma Maandiko yatakayopanua hali yao finyu na kupanua kuelewa kwao. Watu wengi huwa makafiri kwa sababu hawawezi kufahamu siri na uwezo wa Mungu. Ufunguo pekee kwetu kwa siri zinazotuzunguka ni kuukiri kuweko na uwezo wa Mungu. Watu lazima wamtambue Mungu kuwa ni Mwumbaji wa ulimwengu. Anayeamuru kutendeka vitu vyote.TVV 339.3

  Kristo aliwatangazia wasikilizaji wake kwamba, kama pasingekuwako na ufufuo wa wafu, Maandiko wanayosema kuwa wanayafuata yasingalikuwa na maana yo yote. Akasema: “Lakini kuhusu wafu, hamkusoma alivyosema Mungu wenu: Mimi ni Mungu wa Ibrahim, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Mungu huona kazi yake kana kwamba imekamilika. Wafu wenye thamani wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu nao watatoka makaburini wapate uzima wa milele. Hapo patakuwa na uhusiano wa karibu sana baina ya Mungu na wafu watakatifu waliofufuka. Yeye huchukulia uhusiano kana kwamba tayari upo sasa. Wafu huishi katika yeye.TVV 339.4

  Masadukayo walinyamazishwa. Hakuna neno lililonenwa ambalo lingetumiwa kumshutumu. Hata hivyo Mafarisayo hawakukata tamaa. Walimwomba Mwandishi fulani amwulize maswali, kuhusu amri kuu katika amri kumi za Mungu ni ipi. Walikuwa wakizitukuza amri nne za kwanza zinazoeleza wajibu wa mtu kwa Mungu kuwa ndizo kuu zaidi. Kuliko zile sita zilizohusu wajibu wa mtu kwa mwanadamu mwenzake lakini Yesu alikuwa ameshutumiwa kwa kuziwekea uzito zile amri sita za mwisho zinazoeleza wajibu wa mtu kwa mwenzake dhidi ya zile nne.TVV 340.1

  Mwandishi aliamka na swali: “Ni amri gani iliyo kuu kuliko zote?” Jibu la Kristo lilikuwa wazi. Kwamba, “Amri ya kwanza mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nia yako yote, na kwa nguvu zako zote”. Ya pilli hufanana nayo, nayo ni hii: “Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hukaa amri zote na manabii.”TVV 340.2

  Amri hizi zote huonyesha kanuni ya upendo. Amri ya kwanza haiwezi kushikwa na ya pili kuvunjwa, wala ya pili kushikwa na ya kwanza kuvunjwa. Na pale tu tumpendavyo Mungu kadiri iwezekanavyo, ndivyo itakavyowezekana kumpenda jirani bila upendeleo.TVV 340.3

  Kristo aliwafundisha wasikilizaji wake kuwa amri za Mungu ni za muhimu zote, wala hazitengani. Hakuna ya muhimu kuliko nyingine. Kumpenda Mungu kutadhihirika katika kuzishika amri zake zote.TVV 340.4

  Mwanasheria aliyemuuliza Yesu swali hilo alishangaa. Mbele ya makuhani na wazee alikiri kwa dhati kuwa Yesu alikuwa amefafanua sheria kweli kabisa.TVV 340.5

  Yule mwandishi alikuwa anaelewa kutofaa kitu kwa ibada na sadaka za kuteketeza na umwagaji wa damu katika upatanisho wa dhambi. Kumpenda Mungu na kumtii na kumheshimu mwanadamu bila kuwa na ubinafsi, vilionekana kwake vya maana kuliko kufuata mapokeo haya ya bure. Majibu yake ya kweli yalikuwa tofauti kuliko ya makuhani na wazee. Yesu alimhurumia mwandishi huyu aliyethubutu kumkiri Kristo wazi hivyo. Yesu akamwambia: “Hu mbali na ufalme wa Mungu.”TVV 340.6

  Mafarisayo walikuwa wamemzunguka Yesu alipokuwa akimjibu mwandishi. Sasa aliwauliza: “Mnadhani Kristo ni nani? Ni mwana wa nani?” Swali hili ni la kujua wanavyomdhania, kuwa ni binadamu tu au kama Mwana wa Mungu. Walijibu: “Mwana wa Daudi.” Yesu alipodhihirisha Uungu wake kwa njia ya miujiza, alipowaponya wagonjwa na kuwafufua wafu, watu walikuwa wanajiuliza, “Huyu siye mwana wa Daudi.” Lakini wengi waliomwita Yesu kuwa Mwana wa Daudi hawakuutambua Uungu wake, Mwana wa Daudi alikuwa pia Mwana wa Mungu.TVV 340.7

  Katika kujibu Yesu akasema: “Daudi mwenyewe alisema kwa uweza wa Roho Mtakatifu; “Bwana alimwambia Bwana wangu; Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.TVV 341.1

  Ikiwa Daudi basi alimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake? Hakuna mtu aliyeweza kumjibu neno, wala hakuna mtu aliyethubutu kumwuuliza swali tena.”TVV 341.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents