Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ghadhabu ya Majasusi

    Wanafunzi waliona ghadhabu ya majasusi na kusikia maneno yao ya chuki. Walimwambia Kristo wakitumaini kuwa atapatana nao. Walisema: “Hujui kuwa Mafarisayo walichukizwa, waliposikia usemi huu?”TVV 220.3

    Yesu aliwajibu: “Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni, litang’olewa.” Kila aina ya desturi na mapokeo ambayo hutukuzwa sana na Marabi, hayataweza kufaulu mtihani wa Mungu. Kila aina ya uvumbuzi wa kibinadamu uliowekwa kuwa badala ya sheria ya Mungu, “kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” Soma Mhubiri 12:14.TVV 220.4

    Hata katika wakristo kuna desturi zinazotumika, ambazo hazina msingi wa kweli, ni mapokeo tu ya wazee. Watu hung’ang’ania mapokeo na kuwachukia wale wanaowanyesha makosa. Leo tunapoambiwa kuziangalia amri za Mungu na imani ya Yesu, huona uhasama sawa na ule uliokuwako nyakati za Kristo. Kwa masalio wa Mungu imeandikwa: “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu Kristo ...” Ufunuo 12:17.TVV 220.5

    Lakini “kila pando lisilipandwa na Baba yangu wa mbinguni litang’olewa.” Badala ya wale waitwao kuwa ni baba wa kanisa, Mungu hutuamuru tushike neno la Baba yetu wa mbinguni, Bwana wa mbingu na nchi. Hapa ndio kweli ilipo isiyochanganyika na uongo, “huniabudu bure, wakifundisha mafundisho ambayo ni maagizo va wanadamu.”TVV 220.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents