Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ufufuo wa Uzima

    “Saa inakuja ambayo wote waliomo makaburini watakapoisikia sauti yake, nao watatoka. Waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, nao waliofanya maovu kwa ufufuo wa hukumu.”TVV 113.3

    Nuru ambayo ingewaangazia Waisraeli, ndiyo itaangazia makaburi. Lakini watu hawa walikuwa vipofu tu. Yesu alikuwa anazivunja kanuni za marabi wala hawakuamini.TVV 113.4

    Wakati, na mahali na hali ya kujisikia kwa watu, viliyafanya maneno ya Yesu katika Sanhedrin yawe yenye kupendeza. Wakuu wa dini wa Israeli walikuwa wakimtafuta yule aliyejitangaza kuwa msimamizi wa Israeli. Bwana wa sabato alikuwa anapanga kujibu malaumu ya kuvunja sabato. Washitaki wake walimwangalia kwa ghadhabu, lakini maneno yake yalikuwa hayajibiwi. Alikataa kuingiliwa katika kazi yake na makuhani na marabi. Hakukubali kuwa alikosa.TVV 113.5

    Badala yaYesu kuomba msamaha, aliwakemea kwa kutojua maandiko. Aliwalaumu kwa kulikataa Neno la Mungu; pamoja na kumkataa Yeye pia. Alisema: “Mwayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa mna uzima wa milele ndani yake; hayo ndiyo yanishuhudiayo.”TVV 113.6

    Agano la Kale huangaza utukufu wa Mwana wa Mungu. Mpango mzima wa Yuda ulikuwa wa unabii wa Injili. Tangu wazee wote na mpango wa utoaji wa mali ilikuwa nuru ya mbinguni ikiangaza miguu ya watu kumwelekea Mwokozi. Katika matoleo yote ya sadaka kifo cha Kristo kilikuwa kinaonyeshwa katika uvumba uliokuwa ukitolewa haki ya Kristo ilionyeshwa. Katika siri ya patakatifu na patakatifu mno, utukufu wake ulikuwako.TVV 113.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents