Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    7 — Mtoto Yesu

    Utoto na ujana wa Yesu uliishia katika kijiji kidogo cha milimani cha Nazareti. Alikulia katika kijiji cha mtu mashuhuri, mwenye ufundi wa vitu vya useremala, akitukuka katika kijiji cha Nazareti kisichokuwa na sifa nzuri.TVV 33.1

    Mtoto alikua na kuongezeka nguvu za mwili na za kiroho pia, akiwa na hekima, maana neema ya Mungu ilikuwa pamoja naye. Luka 2:52 Mawazo yake yalikuwa wazi sana yenye kuwaza kamili kupita umri aliokua nao. Uwezo wake wa mwili na akili viliongezeka kabisa katika hali yake ya kitoto.TVV 33.2

    Tangu utoto wake Yesu alionyesha tabia ya kupenda mambo manyofu, uvumilivu, kutokuwa na harara wala wasiwasi, hakuwa na mashaka kwa lolote. Alisimama katika kanuni bila kutikisika. Maisha yake hayakuwa ya ubinafsi hata kidogo.TVV 33.3

    Mama yake aliangalia jinsi Yesu alivyoendelea na hali yake, naye akamtia moyo kuendeleza hali bora hiyo. Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mariamu alipata hekima ya kumwongoza Yesu katika tabia hiyo. Naye alimtambua Mungu kama Baba yake.TVV 33.4

    Siku hizo Kristo alipokuwa mtoto, mafundisho ya vijana yalikuwa ya bora mradi tu. Mapokeo yalikuwa yamechukua mahali pa maandiko matakatifu.TVV 33.5

    Mawazo ya vijana yalijazwa na mambo ya uchumi tu, ambayo hayakutambuliwa huko mbinguni kuwa ndiyo mafundisho yafaayo. Wanafunzi hawakupata nafasi ya kuzungumza na Mungu wakiwa katika hali ya ukimya ili wasikie sauti yake ikinena nao kimya. Kwa hiyo wakajitenga na kisima cha hekima. Yale yaliyodhaniwa kuwa ndiyo mafundisho muhimu, yalikuwa sumu mbaya kuzuia maendeleo ya vijana. Mawazo yao yalidumaa na kufinyika.TVV 33.6

    Mtoto Yesu hakupata mafundisho katika masinagogi yaliyokuwa yakiendesha shule. Mama yake alimfundisha mambo ya manabii, ambayo ni maandiko matakatifu. Alivyoendelea kukua, hakutaka kutafuta mafundisho yaliyokuwa yakitolewa na walimu wa Kiyahudi. Hakupenda mafundisho ya jinsi hiyo. Ujuzi wake katika mambo matakafifu wakati wa utoto wake, ulionyesha jinsi alivyopenda kujifunza neno la Mungu.TVV 34.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents