Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uchungu Wa Mama Wa Kristo

    Katika mahali pa kusulibishiwa, wale wezi wawili walishindana sana na watu waliowawamba misalabani; lakini Yesu hakushindana. Mama wa Yesu akitegemezwa na Yohana amemfuata nyayo za mwanaye mpaka Kalwari. Alitamani sana kuweka mikono yake chini ya kichwa chake kilichojeruhiwa lakini hakupata nafasi hii ya kuomboleza. Bado alitazamia kuwa Yesu atajiokoa mwenyewe kutoka kwa watesi wake. Mara roho yake ilizimia alipokumbuka kwamba Yesu alitabiri matukio yaliyokuwa yanatendeka sasa.TVV 422.1

    Wale wezi walipokuwa wanafungwa msalabani aliangalia kwa wasi wasi wa uchungu. Je! yeye aliyewapa wafu uhai mwenyewe ataruhusu asulibishwe. Je! lazima atupe imani yake kwamba ni Masihi? Aliona mikono yake ikinyooshwa juu ya msalaba nyundo na misumari vililetwa, na wakati misumari ilipopigiliwa katika nyama nyororo wanafunzi walimwondoa mama yake Yesu kutoka pale akiwa amezimia.TVV 422.2

    Mwokozi hakulalamika, lakini matone makubwa ya jasho yalionekana usoni pake. Hapakuwapo na mkono wenye huruma kuweza kufuta umande wa mauti kutoka katika uso wake; maneno yenye huruma na uaminifu kutuliza moyo wake wa kibinadamu. Wakati askari walipokuwa wakitenda kazi yao ya kuogofya Yesu aliomba, “Baba uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo.” Mawazo yake yalipita kutoka katika yale yaliyokuwa, yanamsibu hadi malipo yatakayokuwa sehemu yao. Hakuna laana iliyowashukia askari hao, waliokuwa wanamtendea ukatili, wala hakuwa kulipiza kisasi kulikotajwa juu ya makuhani na wakuu. Alipumua tu ombi la msamaha kwa ajili yao “maana hawajui watendalo.”TVV 422.3

    Lakini kutofahamu kwao haukuwaondolea hatia yao, kwa sababu ilikuwa nafasi yao kumfahamu na kumpokea Yesu kama Mwokozi wao. Baadhi yao wangeona dhambi zao, watubu na kuongoka. Wengine kwa ukaidi wao wangedumu kuwa hivyo na kufanya sala ya Yesu isijibiwe kwa ajili yao. Hata hivyo, kusudi la Mungu lilikuwa linafikia utimilifu wake. Yesu alikuwa anapokea haki ya mwombezi wa wanadamu mbele za Baba.TVV 422.4

    Lile ombi la Kristo kwa adui zake lilimhusu kila mwenye dhambi, tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka mwisho wa nyakati. Watu wote wanahusika na kusulubishwa kwa Mwana wa Mungu. Msamaha hutolewa kwa wote bure.TVV 422.5

    Mara tu baada ya Yesu kuambwa msalabani, msalaba ulinyanyuliwa na watu wenye nguvu ukasimikwa kwa kishindo katika shimo lililoandaliwa. Hali hii ilisababisha maumivu makali sana. Kisha Pilato aliandika anwani kwa Kiebrania, Kigiriki na Kilatini, akaiweka msalabani juu ya kichwa cha Yesu. Anwani hiyo ilisomeka hivi, “YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI.” Jambo hili liliwachukiza Wayahudi waliopiga kelele, “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.” Lakini Pilato aliandika yale waliyosema. Hakuna kosa lo lote lililotajwa, isipokuwa kwamba Yesu alikuwa Mfalme wa Wayahudi, ukubali wa dhati kwamba waliapa utii, kwa Warumi. Hii ilitangaza kuwa ye yote atakayejitangaza kuwa mfalme wa Israeli atapata hukumu ya kifo. Katika juhudi ya kumwangamiza Kristo, makuhani walikuwa tayari hata kupoteza jadi ya taifa lao.TVV 423.1

    Makuhani walimwomba Pilato abadili maandiko hayo yasiwe kwamba: “Mfalme wa Wayahudi;” bali ya kwamba yeye alisema; “Mimi ni mfalme wa Wayahudi.” Lakini Pilato akiwa na ghadhabu, alijibu bila kujali “Nilivyoandika, nimeyaandika.”TVV 423.2

    Kwa majaliwa ya Mungu maandiko hayo yalikusudiwa kuamsha shauku ya kuchunguza Maandiko Matakatifu. Watu kutoka pande zote walifika Yerusalemu, na tangazo hilo likitaja Yesu kuwa ndiye Masihi, lingeonekana na kusomeka nao. Tangazo hilo liliandikwa kwa uongozi wa Mungu.TVV 423.3

    Katika mateso ya Kristo msalabani, unabii huu ulitimia, “Kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizuia mikono na miguu” “Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura.” Zaburi 22:16-18. Nguo zake zilipewa askari. Koti lake lilifumwa bila upindo au mshono, basi wakaambiana “Tusilipasue, lakini tulipigie kura liwe la nani.”TVV 423.4

    Katika unabii mwingine Mwokozi alisema; “Nikangoja aje wa kuhurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu. Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakanimywesha siki.” Zaburi 69:20, 21. Kwa wale waliohukumiwa kifo cha msalaba walikuwa wakinyweshwa aina ya siki kuwafanya wasisikie maumivu makali. Lakini Yesu alipoionja alikataa. Imani yake lazima iwe kwa Mungu tegemeo lake la pekee. Kufifisha akili zake kungetoa nafasi kwa Shetani. Makuhani, wakuu na waandishi waliungana na makutano kumdhihaki Mwokozi aliyekuwa anakufa. Sauti ya Baba kutoka mbinguni kumshuhudia Kristo kuwa ni Mungu ilikuwa kimya. Hakuna ushuhuda wo wote kwa ajili yake uliosikika. Aliteseka peke yake.TVV 423.5

    Watu walisema; “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani.” “Na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo Mwana wa Mungu mteule wake.” Shetani na malaika zake wakiwa katika mfano wa wanadamu walikuwako pale msalabani wakiungana na makuhani na wakuu katika dhihaka hizi za wazimu.TVV 424.1

    Yesu aliwasikia makuhani wakitangaza “Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye Kristo Mfalme wa Israeli na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.” Kristo angeweza kushuka kutoka msalabani. Lakini kwa sababu hakujiokoa mwenyewe mwenye, dhambi analo tumaini la msamaha wa dhambi na kukubalika na Mungu.TVV 424.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents