Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Nabii Danieli Alitabiri Kazi ya Kristo

    Mzigo wa mahubiri ya Kristo ulikuwa: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni mkaiamini Injili.” Marko 1:1 5. Ujumbe wa Injili kama ulivyosemwa na Mwokozi, ulijengwa juu ya unabii. “Wakati” ambao alisema kuwa umetimia, ulikuwa muda ule aliofunuliwa Danieli. “Majuma sabini yamekusudiwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha uasi, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho wa maovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri njozi na unabii, na kumtia mafuta Mtakatifu.” Danieli 9:24. Kwa unabii siku inasimama badala ya mwaka. Ezekiel 4:6. Majuma sabini au siku 490 ni sawa na miaka 490.TVV 124.1

    Mwanzo wa muda huu umeelezwa: “Ujue basi na kufahamu, kuwa tangu kutolewa amri ya kuujenga Yerusalemu hata Masihi Mkuu, utakuwa muda wa majuma saba na muda wa majuma sitini na mawili. Majuma sitini na tisa au miaka 483. Danieli 9:25.TVV 124.2

    Amri ya kuurudisha na kuujenga Yerusalemu, kama ilivyotimizwa kwa amri ya Artashashta Longimanus (Tazama Ezra 6:14; 7:1-9) iliyotolewa mwaka B.C. 457. Tangu wakati huo miaka 483 iliendelea mpaka A.D. 27, kama unabii usemavyo. Muda huu utafika mpaka kwa Masihi, ambaye ni mtiwa mafuta: Mwaka A.D. 27 Yesu alipobatizwa alitiwa mafuta kwa Roho Mtakatifu, na baadaye akaanza kazi yake. Kisha ujumbe ulitangazwa kwamba: “Wakati umetimia.”TVV 124.3

    Kisha malaika alisema: “Kwa juma moja atathibitisha agano kwa wengi (miaka saba). Kwa muda wa miaka saba baada ya Mwokozi kuingia kazini, Injili itatangazwa hasa kwa Wayahudi. Kristo mwenyewe atatangaza injili miaka mitatu na nusu, na mitume miaka iliyobaki.TVV 124.4

    “Kati ya juma atakomesha kafara ya dhabihu.” Danieli 9:27. Katika mwaka A.D. 31 Kristo ambaye ni kafara halisi alitolewa huko Kalwari. Kisha pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kuonyesha kuwa umuhimu wa huduma na kafara za kawaida umeondoka. Wakati umefika wa kukomesha kafara na dhabihu.TVV 124.5

    Juma moja, yaani siku au miaka saba ilimalizika katika mwaka A.D. 34. Ndipo kwa kumpiga Stefano kwa mawe, Wayahudi walitia muhuri kukataa kwao injili. Mitume waliotawanyika kwa ajili ya mateso. “Walienda huko na huko wakilihubiri lile neno.” Matendo 8:4. Baadaye Sauli mtesaji aliongoka, akawa Paulo, mtume kwa watu wa mataifa.TVV 124.6

    Muda wa kuja kwa Kristo, kufa kwake, na kuhubiri injili kwa mataifa vilionyeshwa dhahiri. Iliwapasa Wayahudi waufahamu unabii huu na jinsi ulivyotimia katika kazi ya Yesu. Kufuatana na unabii wa Danieli, Yesu alisema: “Asomaye afahamu.” Mathayo 24:15. Alisema hayo kuhusu wakati wao. Baada ya kufufuka kwake, alieleza kwa wanafunzi wake: “Unabii wote unaomhusu yeye.” Luka 24:27. Mwokozi alikuwa amesema kwa njia ya manabii, akishuhudia kabla na mateso yake na utukufu utakaofunuliwa baadaye. 1 Petro 1:11. Alikuwa Gabrieli, malaika mkuu, aliyekuja kumfunulia Danieli. Malaika huyu huyu ndiye alitumwa na Kristo kwenda kumfunulia Yohana mambo ya Ufunuo. Uheri umesemwa kwa wale wenye kusoma maneno ya unabii na kuyashika mambo yaliyoandikwa humo, Ufunuo 1:3. Mungu atawabariki wenye kutii, wakisoma unabii kwa unyenyekevu kwa roho ya maombi.TVV 125.1

    Kwa ujumbe kwa kuzaliwa kwa Kristo ulivyotangazwa, ambao ulikuwa ni ujumbe wa neema, ndivyo na ujumbe wa kurudi kwake kwa utukufu utakavyotangazwa. Ujumbe huu wa pili, sawa na ule wa kwanza, umejengwa juu ya unabii. Mwokozi mwenyewe ametoa unabii kuhusu kurudi kwake kwa kuonyesha dalili nyingi. Amesema: “Jiangalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulevi na ulafi, na masumbuko ya dunia hii, hata siku ile iwaghafilishe kama mtego unasavyo.” “Kesheni basi, na kuomba daima, ili mhesabiwe kuwa mnastahili, mambo haya yatakapotokea, mpate kusimama mbele ya Mwana wa Adamu ajapo.” Luka 21:34, 36.TVV 125.2

    Wayahudi waliutafsiri unabii kimakosa, na wala hawakujua wakati wa kujiliwa kwao. Miaka ya kazi ya Kristo na ya mitume Wayahudi walishughulika kupanga namna ya kuwaangamiza tu wajumbe wa Mungu. Anasa za dunia na kutafuta makuu ya dunia hii kumewapumbaza watu wengi, hata hawaoni mambo yanayotimiza unabii yatokeayo kwa haraka sana, na dalili za kuja kwake zinazoharakisha mno, zikitangaza kuja kwa ufalme wa Mungu. Ingawa hatujui siku kamili ya kuja kwa Bwana, tunaweza kujua jinsi ilivyokaribia sana. “Kwa hiyo tusilale usingizi kama wengine; ila tukeshe na kuwa na kiasi.” 1 Wathesalonike 5:6.TVV 125.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents