Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hekalu latakaswa kwa kuwako kwake Bwana

    Watu wote walioona uwezo huu walitaharuki. Hata wanafunzi wake walitetemeka. Hali ya maneno ya Yesu vilitia hofu sana, na watu wakawa na uchaji kamili. Walikumbuka kuwa iliandikwa kuhusiana na hili kwamba, “Wivu wa nyumba yako, umenila.” Zaburi 69:9. Baadaye uwanja wa hekalu haukufanyiwa biashara tena. Watu walitulia kabisa. Kuwako kwake Bwana kumeleta utakaso wa hekalu, na heshima ipasayo kuonyeshwa.TVV 82.3

    Katika kutakasa hekalu, Yesu alitangaza kazi yake, ya kuwa ndiye Masihi, na akaingia katika kazi mara moja kwa dhahiri. Hekalu lilikusudiwa kuwa fundisho kwa Waisraeli na kwa ulimwengu pia. Mungu alikusudia ya kuwa kila kiumbe kiwe hekalu la kiroho la makao ya Mwumbaji. Kwa ajili ya kuchafuliwa na dhambi, mioyo ya watu haikuwa makao ya Mwenyezi Mungu tena. Lakini wa kule kufanyika mwili kwa Mwana wa Mungu, Mungu huishi katika ubinadamu, na kwa ajili ya neema yake, mioyo ya watu huwa makao yake tena. Mungu alikusudia kuwa hekalu la Yerusalemu, lingeendelea kushuhudia ukuu uliofunguliwa kwa ajili ya watu wote. Lakini Wayahudi hawakujitolea kuwa hekalu takatifu la kuwa makao ya Mungu. Uwanja wa hekalu ulitumika kama mahali pa biashara haramu, ukiwakilisha mahekalu yote machafu, ambayo ni mioyo ya watu yenye tamaa na mawazo machafu, isiyofaa kuwa makao ya Roho Mtakatifu.TVV 83.1

    Katika kutakasa hekalu, Yesu alitangaza kazi yake ya kutakasa mioyo ya watu. Kutokana na dhambi; yaani tamaa ya mwili, na kuupenda ulimwengu, na kupenda mazoea mabaya yanayoharibu roho. “‘Bwana mnayemtafuta atakuja ghafla katika hekalu lake; M jumbe wa agano ambaye mnampenda. . . . Lakini nani atastahili siku ya kuja kwake, na ni nani atasimama atakapoonekana? Maana ni kama moto utakasao. . . . Ataketi kama mtakasaji wa fedha, naye atawatakasa wana wa Lawi, kama atakasaye dhahabu na fedha.” Malaki 3:1-3.TVV 83.2

    “Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu hukaa ndani yenu? Mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu pia atamharibu mtu huyo; maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ni ninyi.” 1 Wakorintho 3:16, 17.TVV 83.3

    Mtu hawezi kuondoa maovu yaliyomo moyoni mwake, kwa nguvu zake mwenyewe. Kristo peke yake aweza kutakasa hekalu la roho. Lakini hawezi kumlazimisha mtu ili apate kuingia. Yeye husema: “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake.” Ufunuo 3:20. Kuwako kwake kutatakasa moyo, upate kuwa safi, mtakatifu kwa Bwana, “makao ya Mungu, kwa Roho.” Waefeso 2:22.TVV 83.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents