Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu akishughulikia kesi ya uzinzi

    Yesu aliondoka katika ghasia za mjini na fujo za Marabi akaenda mahali patulivu katika mlima wa mizeituni, mahali ambapo atakuwa na Mungu kwa upweke. Lakini asubuhi yake mapema alirudi hekaluni, na watu wakamkusanyikia.TVV 261.3

    Mara alitiwa fujo. Mafarisayo na Waandishi walifika kwake, huku wakimkokota mwanamke kwa hasira. Walipaza sauti wakisema kuwa wamemfumania mwanamke huyu katika uzinzi. Wakimsukumiza kwa Yesu, walisema: “Musa alituagiza kuwa watu wa namna hii wapigwe mawe. Nawe wasemaje?”TVV 261.4

    Walipata nafasi ya kupitia ili atakavyoamua, wapate sababu ya kumshitaki. Je, atamwachia huyu mwanamke, kama ndivyo watamshitaki kwamba anadharau amri za Musa. Kama akisema kuwa anastahili kupigwa mawe, watamshitaki kwa Warumi kuwa anachukulia sheria ya kuua watu badala ya serikali ya Kirumi.TVV 261.5

    Yesu alitazama mambo haya, mwanamke mbele yake, akitetemeka kwa aibu, wala hana la kujitetea. Akaangalia nyuso za washitaki wake, na kujua maisha yao yalivyo, bila kuonyesha dalili kuwa amesikia swali walilomuuliza, aliinama chini, akaanza kuandika mchangani.TVV 261.6

    Washitaki wale walianza kuwa na wasiwasi kwa ukimya wake, wakaanza kuchukia. Lakini walipotazama chini mahali alipoandika, nyuso zao zilibadilika, maana walisoma siri za maisha yao. Wakaaibika na kuwa na aibu.TVV 261.7

    Marabi hawa waliona kuwa ni wavunja sheria pamoja na heshima yao kama watu wa dini, llipasa mume wa mke huyu ndiye atoe hukumu iwapasayo. Walimtaka Yesu atoe uamuzi wake lakini Yesu alifunua siri za matendo yao maovu.TVV 262.1

    Sheria ilisema kuwa mtu aliyeshuhudia ndiye awe wa kwanza kumpiga jiwe. Yesu sasa alipoinua macho yake na kuwaangalia washitaki wale alisema: “Mtu asiye na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumpiga jiwe.” Akaendelea kuandika.TVV 262.2

    Sasa watu wale walifunuliwa vazi la utakatifu walilojifunika, wakaonekana wako wazi mbele za Mwenyezi wala hawakujificha kitu. Wakaondoka mmoja mmoja wakiwa na aibu, wakaenda zao, wakamwacha yule mwanamke na Yesu peke yake.TVV 262.3

    Yesu akiinua macho yake na kumtazama yule mwanamke, alisema: “Mwanamke, wako wapi washitaki wako? Hakuna aliyekuhukumu? Mwanamke alisema: “Hakuna Bwana.” Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu: Nenda zako, usitende dhambi tena.”TVV 262.4

    Mwanamke alikuwa amesimama mbele ya Yesu akiwa na hofu nyingi. Maneno ya Yesu kuwa “Mtu asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga jiwe”, yalikuwa kama maneno mafu kwa mwanamke. Alingoja kusikia ajali itakayompata. Alishangaa kuwaona washitaki wake wakiondoka kimya kimya, wakifedheheka. Ndipo alisikia maneno yenye matumaini yakisema. “Wala mimi sikuhukumu, nenda zako usitende dhambi tena.” Roho yake ilitulia na kujaa furaha kwa ajili va upendo huo. Aliungama dhambi zake kwa machozi.TVV 262.5

    Kwake huu ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya; matakatifu ya amani. Kwa kumwinua mtu huyu kutoka dhambini Yesu alitenda mwujiza mkubwa, kwamba amemponya mwovu na kumwokoa na kifo. Mwanamke huyu alikuwa mfuasi wa Yesu mashuhuri.TVV 262.6

    Yesu hakuihalalisha dhambi, wala kuihafifisha, ila alitaka kuokoa. Mtu anamhurumia mdhambi na kumwinua toka matopeni ni bora. Sio kazi ya wafuasi wa Kristo kuwaacha wenye dhambi matopeni. Watu huwachukia wenye dhambi, wakati wanapoipenda dhambi. Kristo naye huchukia dhambi na kumpendelea mwenye dhambi. Watu wanaomfuata wangekuwa na roho kama ya Yesu. Wakristo wasipende dhambi, lakini wawapende wenye dhambi, wawe tayari kuwainua na kuwatoa dhambini, na kuwaweka kwa njia ya utakatifu.TVV 262.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents